.

UGANDA YAOMBA MSAADA WA KIMATAIFA KUKABILIANA NA WIMBI LA WAKIMBIZI

Feb 16, 2017

Uganda imeomba kupewa msaada wa kimataifa kwa ajili ya kutatua mgogoro wa wakimbizi wamaomiminika nchini humo.
Waziri wa Misaada, Kukabiliana na Majanga na Wakimbizi wa Uganda, Hillary Onek amesema kuwa, usimamizi wa masuala ya wakimbizi umekuwa mgumu zaidi kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi wanaoingia nchini humo.
Waziri Hillary Onek ameongeza kuwa, Uganda inakabiliwa na ongezeko kubwa la wakimbizi. 
Uganda imewapa hifadhi wakimbizi zaidi ya milioni moja, nusu yao wakiwa ni kutoka nchi jirani ya Sudan Kusini ambako mapigano ya ndani bado yanaendelea. Kwa wastani wakimbizi 4,000 wa Sudan Kusini wanasemekana kuvuka mpaka kila siku na kuingia Uganda.
Mkimbizi katika kambi ya wakimbizi Uganda
Wakimbizi wengine walioko Uganda ni kutoka nchi za Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Eritrea na Ethiopia.
Uganda imesifiwa kimataifa kutokana na sera yake ya kufungua milango kwa wakimbizi wakati nchi nyingi zimefunga milango yao mbele ya wakimbizi wanaokimbia nchi zao kwa ajili ya kuokoa maisha. 

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช