Breaking News

Your Ad Spot

Feb 14, 2017

UN: 100 WAUAWA KATIKA MAPIGAMO KATI YA JESHI NA WAASI DRC

Umoja wa Mataifa umesema jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limeua makumi ya watu katika makabiliano na kundi la waasi kati ya Februari 9 na 13.
Taarifa ya UN iliyotolewa leo Jumanne imesema kuwa, watu 101, wakiwemo wanawake 39 wameuawa katika mapigano hayo makali katikati mwa nchi, baina ya askari wa jeshi la Kongo DR na waasi wa kundi la Kamwina Nsapu, katika mji wa Tshimbulu, yapata kilomita 60 kusini mwa mkoa wa Kananga.
Liz Throssell, msemaji wa shirika la kutetea haki za binadamu amesema mapigano kati ya pande mbili hizo yalianzishwa na kundi hilo la waasi wanaotaka kulipiza kisasi cha kuuawa kamanda wao, Kamwina Nsapu.
Waasi wanaobeba silaha Kongo DR
Nsapu aliuawa mwezi Agosti mwaka jana, baada ya kutishia kuuvamia mkoa wa Kasai ya Kati, akiwatuhumu maafisa usalama kuwa wanawakandamiza raia katika eneo hilo. Tangu baada ya kuuawa Nsapu, miji kadhaa na vijiji vya Kasai ya Kati na Kasai ya Mashariki imekuwa ikisumbuliwa na vurugu, machafuko na mapigano kati ya askari wa kulinda usalama na wanamgambo hao wanaomuunga mkono kiongozi wao huyo wa zamani.
Mapigano yanaripotiwa kukithiri kote Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na hatua ya Rais Joseph Kabila ya kukataa kuondoka madarakani baada ya muhula wake wa urais kumalizika mwezi Disemba mwaka jana.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages