Breaking News

Your Ad Spot

Feb 7, 2017

WAZIRI MKUU AZUNGUMZA NA MABALOZI, AWATAKA WAKATAFUTE WAWEKEZAJI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akizungumza na mabalozi ambao wanaiwakilisha Tanzania nje ya nchi na wanatarajiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi hivi karibuni, Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akizungumza na mabalozi ambao wanaiwakilisha Tanzania nje ya nchi na wanatarajiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi hivi karibuni, Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akizungumza na mabalozi ambao wanaiwakilisha Tanzania nje ya nchi na wanatarajiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi hivi karibuni, Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akizungumza na mabalozi ambao wanaiwakilisha Tanzania nje ya nchi na wanatarajiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi hivi karibuni, Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017. Kutoka kushoto ni Samwel Shelukindo (Ufaransa), Dkt. James Msekela (Uswisi), Mbelwa Kairuki (China), Paul Mella (DRC), Dkt. Emmanuel Nchimbi (Brazil) George Madafa (Italy) na Elizabeth Kiondo (Uturuki).


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akisalimiana na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam,
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akisalimiana na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU )

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali kuhakikisha wanatumia uwakilishi wao kutafuta wawekezaji watakaokuja kuwekeza katika sekta ya viwanda nchini.
Amesema mkakati wa Serikali ni kuimarisha uchumi hadi wa kati kupitia sekta ya viwanda, hivyo jukumu la mabalozi hao ni kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa.


Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Februari 7, 2017) alipokutana na mabalozi wa wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi za Uturuki, Brazil, China, Italy, Ufaransa, Jamuhuri ya Kidemkrasi ya Congo (DRC) na Uswisi.

Mabalozi hao ni Balozi Dk. Emmanuel Nchini (Brazil), Balozi Elizabeth Kiondo (Uturuki), Balozi George Madafa (Italy), Balozi James Msekela (Uswisi),Balozi Samuel Shelukindo (Ufaransa), Balozi Paul Mella (DRC), Balozi Mbelwa Kairuki (China).

“Serikali inahitaji watu wa kuja kuwekeza katika viwanda ili kuongeza thamani ya mazao kabla ya kuyauza nje ya nchi, hivyo jukumu lenu ni kuhakikisha tunapata wawekezaji wenye sifa,” amesema.

Pia Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao kutumia uwakilishi wao katika nchi hizo kwa kuhakikisha wanatangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kuongeza idadi ya watalii wanaokuja Tanzania.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao kulinda maslahi ya Taifa katika nchi hizo ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na mataifa hayo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao kuhakikisha wanawatambua Watanzania wanaoishi katika mataifa hayo na kushirikiana nao katika kutafuta wawekezaji wa kuja kuwekeza nchini.

Kwa upande wake Balozi Mella ambaye alizungumza kwa niaba ya mabozi wenzake alimuhakikishia Waziri Mkuu kwamba watakwenda kutekeleza wajibu wao ipasavyo.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMANNE, FEBRUARI 7, 2017.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages