Breaking News

Your Ad Spot

Feb 11, 2017

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA MAZOEZI YA VIUNGO KWA WANANCHI WOTE MJINI DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (aliyevaa traksuti nyeusi) akiwa ameongozana na Viongozi mbalimbali kuelekea Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwenye Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (aliyevaa traksuti nyeupe) akiwa ameongozana na Viongozi mbalimbali kuelekea Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwenye Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma

Kikosi cha Bendi ya Matarumbeta ycha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiongoza matembezo kuelekea Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwenye Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017.

Umati wa watu pamoja na Jeshi la Wananchi Tanzania wakiwa katika matembezi kuelekea Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwenye Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma .
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wa pili kulia), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) pamoja na Viongozi wengine wakifanya mazoezi kuelekea Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwenye Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (aliyevaa traksuti nyeupe) akiongoza mazoezi ya viungo wakati wa Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwahutubia baadhi ya Viongozi wa Serikali pamoja na wananchi (hawapo pichani) waliohudhuria Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akitoa neno la shukrani mbele ya Viongozi wa Serikali pamoja na wananchi waliohudhuria Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma .

Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiongelea kuhusu umuhimu wa mazoezi katika kulinda afya, mbele ya Viongozi wa Serikali pamoja na wananchi waliohudhuria Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma .

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu(Vijana, Kazi na Ajira), Mhe. Anthony Mavunde, akiongea jambo akiwa kama Kiongozi mwakilishi wa Mkoa wa Dodoma, mbele ya Viongozi wa Serikali pamoja na wananchi waliohudhuria Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo leo mara baada ya kumalizika kwa Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma .
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)

Na. Lilian Lundo-Dodoma.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ameziagiza Halmashauri, Manispaa na Majiji yote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya wananchi kufanya mazoezi na kupumzika.
Kassim Majaliwa ametoa agizo hilo leo, Mjini Dodoma wakati wa Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri.

"Ni muhimu kufanya mazoezi kila siku, mazoezi yanasaidia kuchangamsha mwili, kufahamiana, kujenga urafiki pamoja na kuwa na afya bora," alisema Mhe. Majaliwa.

Waziri Mkuu amesema kwamba, muitikio wa ufanyaji mazoezi wa viungo ni mkubwa, ambapo watu wengi wamejiunga na vikundi mbalimbali vya kufanya mazoezi ya viungo.

Aidha, amezitaka Halmashauri, Manispaa na Majiji yote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya watu kufanya mazoezi na kumpuzika.
Ameongeza kuwa, watu wasilazimishwe kufanya mazoezi bali iwe ni hiari ya yao na kusiwe na gharama kwa ajili ya mtu kufanya mazoezi.

Vile vile amewataka Maafisa Utamaduni na Michezo nchini kuhamasisha mazoezi ya viungo katika maeneo yao pamoja na kuanzisha vikundi vya mazoezi ya viungo ambapo watakuwa wanakutana na kufanya mazoezi kwa muda ambao watajipangia.
Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemshukuru Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuhamasisha mazoezi ya viungo na kuitangaza rasmi Jumamosi ya pili ya kila mwezi kuwa ni siku ya mazoezi ya viungo Kitaifa.
Aliendelea kwa kusema kuwa, mazoezi ya viungo yanamuepusha mtu na kupata magonjwa yasiyoambukiza kama vile magonjwa ya moyo, kisukari pamoja na saratani.

Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amesema kwamba, mazoezi ya viungo yanaratibiwa na Wizara ya Habari, Wizara ya Afya pamoja na TAMISEMI. Hivyo kwa pamoja watahamasisha uanzishwaji wa vikundi vya mazoezi ya viungo katika Halmashauri zote nchini kwa kuanza na watumishi wa Umma.

Aidha amewataka viongozi wanapokuwa mikoani katika siku ya mazoezi ya viungo wawahamasishe wananchi kufanya mazoezi ya viungo kwa ajili ya kulinda afya zao.

Uzinduzi wa Kitaifa wa mazoezi ya viungo ulianza kwa matembezi yaliongozwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuanzia viwanja vya Bunge na baadaye alimkabidhi Waziri Mkuu kuanzia Nyerere Square mpaka Uwanja wa Jamhuri. Uzinduzi huo umehusisha viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Viongozi wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Wananchi wa Mkoa huo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages