Breaking News

Your Ad Spot

Mar 4, 2017

MUATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA AANDAA JENEZA NA KUCHIMBA KABURI AKIFA AZIKWE HAPO


Nafahamu umeshakutana na habari nyingi za watu ambao hutoa maagizo kwa ndugu zao kwamba siku wakifa wazikwe kwa majeneza gani au kuchagua sehemu za kuzikwa, leo nakukutanisha na hii ya Dubliner John Edwards, 61.
Huyu ni raia wa Ireland Kaskazini ambaye ni muathirika wa dawa za kulevya, naambiwa ameamua kuchimba kaburi lake na kutengeneza Jeneza ili siku akifa azikwe hapo.
Edwards, ambaye amepoteza zaidi ya marafiki zake 20, baadhi yao kwa kujiua kutokana na dawa za kulevya, kupitia kile alichosema: “Kukutana na ajabu ya Mungu miaka 27 iliyopita”, ameamua kuanzisha kituo cha kikristo kitoacho huduma ya malazi na makazi kwa ajili ya watu hao.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages