Breaking News

Your Ad Spot

Mar 7, 2017

WANAWAKE ACHENI UNYANYASAJI KWA WAUME ZENU NA WADADA WA KAZI-KIGOMA

Na Magreth Magosso.Kigoma 

WANAWAKE Nchini wametakiwa waache tabia ya unyanyasaji kwa waume zao na wasichana wa kazi za ndani licha ya kutambuliwa kuwa ni miongoni mwa wahanga wa vitendo vya ukatili dhidi ya mila na desturi na jamii ya jinsi ya kiume.

 Pia wametakiwa wajitambue uwepo wao kunaazia ngazi ya familia  kwa kulea watoto katika maadili mema bila ubaguzi , ingawa bado wanaendelea kudai haki zao za msingi hasa usawa katika umilikishwaji wa mali, nyadhifa na heshima katika jamii, lakini waache kunyanyasa wenzao. 

 Hayo yalibainika juzi kwenye madhimisho ya wanawake wa kikristo yaliyofanyika katika Kanisa la Babtisti wilayani kibondo mkoani kigoma,uliolenga kuombea changamoto za ukatili wa kijinsia hasa wanawake ambao ndio wahanga wakubwa wa matukio ya ubakwaji,vipigo,kuuwawa na rushwa ya ngono ili kutimiza ndoto zao. 

 Akithibitisha kauli hiyo Mwenyekiti wa wanawake hao Mkoa wa Tabora Justa Saulo alisema changamoto kubwa ipo kwa wanawake wenyewe kutojitambua katika ngazi ya familia hali inayochangiwa na matukio ya unyanyasaji kushamiri katika familia husika.

 Alisema kitendo cha kuwafanyia madhira kadhaa waume zao sanjari na wadada wa kazi za ndani ni kikwazo cha wao kujinasua na haki waitakayo, kuwa wameshindwa kulinda na kuenzi ndoa zao huku wakitoa vipigo visivyo na tija kwa wadada hao sambamba na kuwanyima mishahara na kuwakata mishahara pindi wanapovunja vyombo vya bahati mbaya. 

Alifafanua kuwa,pamoja na juhudi kubwa inayofanywa na mataifa mbalimbali duniani lakini imebainika wanawake wanaongoza kufanya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa asilimia kubwa ukilinganisha na upande wa pili ilihali wao ni walezi katika familia husika . 

 Saulo alisisitiza kuwa,wanawake hawana budi wajitazame kwa jicho la tatu dhidi ya matukio ya ubakwaji na rushwa ya ngono na waepuke kuwafanyiwa ukatili wa kuwachoma moto viungo mbalimbali vya watoto na kuwanyima chakula na wawalipe stahiki zao wadada wa kazi na kuwaheshimu pia, ikiwa wanadai haki za usawa mtambukwa. Kwa upande wa Mgeni rasmi Mchunganji wa kanisa la Anglikana Jimbo la kibondo Themeo Ndeza aliwakumbusha wanawake kuwa hakuna mtoto asiye na baba ,hivyo kila mmoja atambue wajibu wake ndani ya familia na maombi ya siku hiyo iwe funguo ya kuimarisha upendo,umoja na mshikamao katika jamii kwa ujumla. 

 Ndeza aliongeza kuwa,pamoja na udhaifu wa wanawake ,wanaume hawana budi kufuata sheria,taratibu za maisha kwa lengo la ustawi wa jamii ndio sababu ulimwengu umetenga siku ya wanawake ili kuibua na kutatua kero zinazowakabili na wanaume wanyanyasaji wachuliwe hatua za kisheria

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages