.

RAIS DK MAGUFULI AKABIDHIWA RIPOTI YA UHAKIKI WA VYETI FEKI, HAKIMO CHA MAKONDA

Apr 28, 2017

KATIBU WA BUNGE AONGOZA KIKAO CHA UONGOZI LEO MJINI DODOMA

 Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Bunge, Ndg. Chacha Nyakega (aliesimama) akifafanua wakati wa kikao cha Management Ofisi ya Bunge kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
 Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah (kulia) akiongoza kikao cha Management Ofisi ya Bunge kilichofanyika leo ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah (katikati) akiongoza kikao cha Management Ofisi ya Bunge kilichofanyika leo ukumbi wa Spika Mjini Dodoma

MIGODI INAYOMILIKIWA NA KAMPUNI YA ACACIA YAWA KIVUTIO KATIKA MAONESHO YA WIKI YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI

Maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya mahala pa kazi yanayofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro.
Maonesho haya yanayohusisha kampuni na Taasisi mbalimbali nchini yanaratibiwa na Wakala wa Usalama na Afya mahala pa Kazi (OSHA).
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,wakiweka sawa moja ya picha inayoonesha eneo ambalo shughuli za uchimbaji unafanyika.
Afisa Uhakiki na Usalama katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA, Amina Mohamed akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,wakitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo katika maeonesho ya wiki ya usalama mahala pa kazi ndani ya viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Afisa Afya katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu ,Tumaini Sylivanus akitoa maelezo ya namna wanavyotoa huduma ya Afya kwa wafanyakazi wa Mgodi huo pindi wapatapo matatizo.
Mmoja wa Wakazi wa Kilimanjaro akipewa maelekezo ya namna ya kutumia kifaa maalumu kinachotumika katika zoezi la uzimaji wa moto pindi yatokeapo majanga ya Moto.Nyuma yake ni mmoja wa wafanyakazi wa Mgodi wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA.
Afisa Viwango wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu,Setieli Kimaro akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliotembelea banda la modi huo unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA.
Afisa Usalama katika Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,Deogratius Nyantabano akitoa maelezo kwa wanafunzi waliotembelea banda la mgodi huo katika maonesho ya wiki ya usalama na afya mahala pa kazi yanyofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ,Kilimanjaro.
Afisa Usalama katika Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,Mustapher Mlewa akieleza jambo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea Banda hilo.
Daktari kutoka Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,Dkt Ludovick Silima akitoa maelezo juu ya usalama kwa mmoja wa wananchi waliofika katika banda la mgodi huo wakati wa maonesho ya wiki ya usalama na afya mahala pa kazi yanayoendelea katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
Afisa Mazingira katika Mgodi wa north Mara ,Sara Cyprian akionesha picha na maelezo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la Mgodi huo katika maonesho ya wiki ya usalama na afya mahala pa kazi.
Afisa Usalama katika mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA,Samweli Nansika (aliyenyoosha kidole) akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la mgodi huo.
Mkuu wa Idara ya Usalama na uokoaji katika Mgodi wa Dhahabu wa North Mara ,Emanuel Erasto(katikati) akitoa maelezo namna amavyo wanaweza kumuokoa mtu aliyepata athari iliytokana na kemikali.
Eneo maalumu la kumuogesha mtu aliyepata athari ya kemikali.
Afisa usalama akita huduma ya kumsafisha mtu aliyepata athali ya kemikali akiwa nje ya bafu hilo la kumuogeshea ili na yeye asipate madhara.
Wafanyakazi wa Mgodi wa Buzwagi wakionesha namna ambavyo wanaweza msaidia mtu aliyepatwa na janga la Moto.
Kifaa Maalumu kinachotumika katika kubeba mwili wa mtu aliyepata madhara akiwa katika shimo wakati wa uchimbaji wa Dhahabu.
Mmoja wa wafanyakazi wa Mgodi wa Bulyanhulu akitoa maelezo kwa wananchi walitembelea banda hilo namna ambavyo wanaweza kunyanyua Gari pamoja na Mawe yaliyomuangukia mtu wakati akitekeleza majukumu yake kwa kutumia kifaa maalumu kinachojazwa upepo (Air Bag).
Mkuu wa Idara ya Usalama na Uokoaji katika Mgodi wa North Mara ,Emanuel Erasto akitoa maelezo namna wanavyoweza kumukoa mtu aliyepatwa madhara akiwa chini ya mgodi .
Dkt Ludovick Silima akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliotembelea banda la Mgodi wa Buzwagi.
Afisa Mahusiano katika Mgodi wa Bulyanhulu akitoa maelezo ya namna Mgodi huo unavyo tekeleza majukumu yake ukitoa kipaumbele katika masuala ya Usalama na Afya kwa watumishi wake.
Afisa Uhusiano wa Mgodi wa Buzwagi ,Magesa Magesa akitoa maelezo namna mgodi huo ulivyoshiriki katika shughuli za maendeleo ikiwemo ujengaji wa vyumba vya madarasa,zahanati,maji pamoja na suala la kuhamasisha michezo katika maeneo yanayozunguka mgodi huo.

Na Dixon Buagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

MAGAZETI YA LEO APRILI 28, 2017

MAGAZETI ZAIDI/>BOFYA HAPA  

SERIKALI: WANAOPATA MIMBA MASOMONI KURUDI SHULENI

Apr 27, 2017

Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu akimuwakilisha Makamu wa Raisi Bi Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa  mkutano wa kwanza wa Masuala ya Usawa wakijinsia  ulioandiliwa na Chuo Cha Ualimu (DUCE) jijini Dar Es salaam
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesisitiza kuwa wanafunzi wa kike wanaopata mimba wakiwa mashuleni waendelee na masomo yao ili kufikia malengo walioyanayo nchini.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa maswala ya kijinsia ulioandiliwa na Chuo Cha Ualimu (DUCE) alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri8 ya Muungano waq Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo jijini Dar es salaam.

“Tunapokataza watoto wa kike wasiendelee na masomo pindi wanapopata ujauzito wakiwa mashuleni  tunawaadhibu watoto wa masikini washindwe kutimiza malengo yao kwa wakati waliotarajia” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa anaunga mkono uamuzi wa  Rais wa Tanzania Dkt. Jonh Pombe  Magufuli kwa  kutoa elimu bure nchini kwani kunaongeza idadi ya watoto wa kike  kuwepo mashuleni tofauti na kipindi cha nyuma.

Mbali na hayo Waziri Ummy ametoa wito kwa wazazi kuwahamasisha watoto wao wa kike kupenda masomo ya sayansi ili kukuza rasilimali watu katika kujenga uchumi unaotokana na viwanda nchini.

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha DUCE Prof. William Anangisye amesema kuwa lengo la  mkutano huo ni kuleta chachu ya kuwatia moyo wanafunzi wa kike kupenda  masomo ya sayansi ili kupata  wanasayansi wanawake nchini.

RAIS DK. MAGUFULI KUWA MGENI RASMI MAADHIMSHO YA SIKU YA UHURU WA HABARI

Na Mwandishi Wetu
Rais Dk. John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Habari, yaliyopangwa kufanyikamwezi Mei mwaka huu.

Maadhimisho hayo ya mwaka huu, yatafanyikia jijini Mwanza kwa Siku mbili mfululizo kuanzia Mei 2 na 3 mwaka huu yakiwa na maudhui yanayosema 'fikra yakinifu kwa wakati muhimu'.


Akizungumzia madhimisho hayo, Mwenyekiti wa Misa Tanzania Salome Kitomary amesema lengo la siku hiyo ni kuwakutanisha wadau wa Habari kuweka msukomo wa mataifa kutunga sheria za vyombo vya habari ambazo zinahakikisha Uhuru wa habari katika nchi husika.


Amesema lengo lingine ni kufikia makubaliano ya kitaifa juu ya kuanzisha utaratibu wa usalama na ulinzi wa wanahabari na wafanyakazi wa vyombo vya habari kwenye mtandao na nje ya mtandao.


Kitomari amesema lengo lingine ni kutetea Sera na mfumo wa mageuzi ya kisheria kwa ajili ya vyombo vya Habari na maendeleo endelevu.


Kwa upande wake Makamu wa Rais kutoka umoja wa Clabu za waandishi Tanzania, UTPC, Janne Mihanji amewataka waandishi wawe ndio wapangaji wa ajenda za taifa badala ya kutumiwa na wanasiasa.


Aidha amewaasa waandishi wakiwa katika maeneo yao kazi, kuchukua tahadhari wakiangalia usalama wao zaidi kwani hakuna habari bora kuliko uhai wa mtu mwenyewe.

KIONGOZI WA UPINZANI NCHINI ZAMBIA KUFUNGWA JELA AU KUNYONGWA

Mahakama nchini Zambia leo imekataa kufuta mashitaka ya uhaini dhidi ya kiongozi wa upinzani, Hakainde Hichilema, kesi ambayo imezusha wasiwasi wa kisiasa miezi kadhaa baada ya uchaguzi nchini humo uliobishaniwa.

Kiongozi huyo wa  chama cha United Party for National Development (UPND) alikamatwa  katika  msako  wa  polisi  nyumbani kwake mwezi  huu na  alifunguliwa  mashitaka  ya  kujaribu  kuipindua  serikali baada ya kufikishwa katika  mahakama  kuu. 

Mawakili  wa  Hichilema wamekata rufaa, wakisema  madai  hayo  hayaeleweki, lakini  jaji  Greenwell Malumani  aliiambia  Mahakama  iliyokuwa  imejaa  watu  kwamba  mahakama  hiyo  haina  mamlaka  ya kufuta madai  hayo na  kuipeleka  kesi  hiyo katika  mahakama  kuu.

Zambia  ilikuwa  moja  kati  ya  nchi  zenye utulivu  mkubwa  katika  eneo  la  kusini  mwa  Afrika  hadi  pale  mahusiano yalipoharibika  kati  ya  serikali  na  upinzani mwezi  Agosti, wakati  chama  cha  Rais  Edgar Lungu  cha  Patriotic  Front  kukishinda chama  cha  UPND katika  uchaguzi ulioelezwa kugubikwa  na  machafuko.
Source: Reuters/R. Ward

WANAOKWENDA HOSPITALI YA KITETE KUONA WAGONJWA WAONDOKANA NA ADHA YA KUKOSA ENEO LA KUSUBIRIA

Wananchi wa Mkoa wa Tabora wanakwenda kuona wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kitete wameondokana na adha ya muda mrefu ya kunyeshewa mvua na kukaa juani baada ya kukamilika na kuzinduliwa kwa Jengo la Mahali pa Kungonjea kuona wagonjwa.

Jengo hilo lililojengwa na Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Tabora na umegharimu shilingi milioni 18 hadi kukamilika.

Uzinduzi huo umefanywa leo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Queen Mlozi wakati wa sherehe fupi zilzofanyika katika Hospiali ya Rufaa ya Mkoa huo Kitete.

Alisema kuwa kukamilika  kwa jengo hilo kwa muda kumesaidia kuondoa kilio cha muda mrefu cha viongozi na wananchi cha kutaka lijengwe eneo la watu kupumuzika wakati wakisubiri muda wa kuona wagonjwa wao wanapata matibabu katika Hosptali hiyo.

Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora aliipongeza Seketarieti ya Mkoa wa Tabora kwa kuwa wabuni hadi kufanikisha ujenzi huo kwa kiwango cha juu na gharama nafuu.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara alisema kuwa ujenzi wa jengo hilo umefanywa kwa kutumia fedha za usimamizi wa miradi ambapo Seketarieti ya Mkoa huo imepunguza katika fedha zake za kufuatilia miradi.

Alisema kuwa hatua hiyo imesaidia kupatikana kwa fedha hizo zilizosaidia kukamilisha kwa jengo ambalo ambalo litasiadia kuepusha wananchi hao na hatari za kugongwa na baiskeli au pikipiki kutokana na kukaa kando kando ya barabara.

Katibu Tawala huyo wa Mkoa aliongeza kuwa kabla ya ujenzi huo walitaka kumtumia Mhandisi kutoka nje ambapo alidai apatiwe shilingi milioni 35 ili afanikishe ujenzi huo , lakini walipoamua kutumia mwandishi wa ndani wameokoa kiasi cha milioni 17.

Aidha , Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora ametoa wito kwa Wakurugenzi wote Watendaji wa Halmashauri nane(8) za mkoani Tabora kuhakikisha wanajenga jengo kwa kila Hospitali la Mahali pa wananchi kuongejea kuona wagonjwa wao.

Alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuwaondelea kero wananchi na kutekeleza ahadi ya Serikali ya awamu ya tano ya kuwajali wanyonge.

Aidha , Dkt. Ntara aliwaahidi wananchi kuwa baada ya kukamilika kwa jengo hilo atajitadi kuwanunulia runinga ili wanapokuwa wanasubiri kuona wagonjwa wafutilie taarifa mbalimbali za habari zinaendelea za ndani na nje ya nchi.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala huyo wa Mkoa wa Tabora wanatarajia kujenga Kliniki mbili katika eneo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kitete kwa ajili ya vijana na wakinamama.

Alisema kuwa lengo la kutaka kufanya hivyo ni kutaka kutoa elimu kwa vijana hasa mabinti kwa ajili ya kupunguza ndoa na mimba za utotoni mkoani Tabora.
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete ilijengwa katika miaka ya 1909 lakini ilikuwa haina sehemu ya watu kukaa wakati wakisiburi kuona wagonjwa.

TGGA YAZINDUA UPANDAJI MITI 600 KILA MKOA TANZANIA

 Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari Mtumba Manispaa ya Dodoma wakiwa na miche ya miti kila mmoja wao kabla ya kuipanda kwenye uzinduzi wa upandaji miti uliofanywa kitaifa na Girl Guides Tanzania mkoani humo. PICHA NA JOHN BANDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

John Banda, Dodoma

CHAMA cha Tanzania Girl Guides (TGGA) kimezindua mradi wa upandaji miti kitaifa katika Shule ya Msingi ya Mtumba Manispaa ya Dodoma kwa lengo la kuifanya nchi kuwa ya kijani ili kuweza kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza katika uzinduzi huo Kamishna Mkuu wa Tanzania Girl Guides nchini, Simphorosa Hangi  alisema wanakamilisha uzinduzi huo  wa kitaifa huku tayari shirika hilo likiwa limeshaanza upandaji wa miti hiyo katika mikoa mingine ya  Arusha, Lindi na Mwanza


Hangi alisema kuwa kwa sasa wapo katika mikoa 22 na wanaendelea kufanya juhudi ili waweze kukamailisha mikoa yote ikiwemo Zanzibar ambapo kila mkoa watapanda miti 600 huku wakiacha kila mkoa kuendelea na zoezi hilo ili kulifanya Taifa kuwa la kijani.


Naye Mwenyekiti wa Shirika hilo kitaifa, Martha Qorro  Alisema zoezi hilo linafanyika mashuleni na kuachwa kwa viongozi wa Girl Guides wa mkoa husika ambao watahakikisha wanapeleka na kupanda miti katika shule ambazo maji yapo yakutosha ili kuifanya miti hiyo kukua.


Kwa upande wake Mgeni Rasmi Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma, Aziza Mumba katika uzinduzi huo alisema juhudi hizo zinazofanywa na Shirika hilo zinafaa kuigwa ili kusaidia kurejesha uoto wa kijani ambao utasaidia kuyaweka mazingira kuwa mazuri yenye rutuba ya kutosha kutokana na mvua zitakazokuwa zikinyesha kila mahali    Wanachama wa Tanzania Girl Guides wakichimba moja ya mashimo ya kupanda mti katika Shule ya Msingi Mtumba Manispaa ya Dodoma wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti katika shule mbalimbali nchini.


 Wanafunzi wanachama wa TGGA
 Wasanii wakitumbuiza kwa ngoma ya kabila la Wagogo wakati wa uzinduzi wa upandaji miti shuleni hapo
 Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma, Aziza Mumba akipanda mti katika Shule ya Msingi Mtumba wakati wa uzinduzi wa upandaji miti uliofanyika kitaifa shuleni hapo juzi.


 Mwenyekiti wa TGGA, Marha Qorro akimwagilia mti baada ya kuupanda


 Viongozi na wanachama wa TGGA wakiwa katika picha ya pamoja
 Viongozi wa TGGA Makao Makuu Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Dodoma
 Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wanachama wa TGGA
Wanafunzi wanachama wa TGGA wakiwa na miche ili waendelee na zoezi la kupanda miti shuleni hapo
ยช