.

RAIS DK. MAGUFULI KESHO KUPOKEA TAARIFA YA MCHANGA WA MADINI ULIKO KATIKA MAKONTENA

May 23, 2017

Ikulu, Dar es Salaam
Rais John Magufuli kesho atapokea Taarifa ya Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza mchanga ulio katika makontena ya mchanga wa madini (Makinikia) yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini Tanzania.

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, imesema leo kwamba, tukio la kupokea taarifa hiyo litahudhuriwa na viongozi mbalimbali na kurushwa moja kwa moja kupitia vituo vya habari vya redio, televisheni na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz

"Wananchi mnakaribishwa kutazama na kusikiliza matangazo hayo yatakayorushwa hewani kuanzia saa 3.30 Asubuhi kutoka Ikulu Jijini Dar es Salaam", imesema taarifa hiyo.

JPM AMTEUA NDUNGURU KUWA NAIBU MKURUGENZI MKUU TRA

Ikulu, Dar es Salaam
Rais Dk. John Magufuli amemteua Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Kamishna wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, anachukua nafasi iliyoachwa na Charles Edward Kichere ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa TRA.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema, uteuzi wa Adolf Hyasinth Mohondela Ndunguru umeanza jana, Mei 22, 2017.

NEEC, UN NA HDIF WAZINDUA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALIKatibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji,Bengi Issa, akizungumza na waandishi wa habarai Dar es Salaam jana wakati wa semina kwa vijana kuhusu namna ya kutumia Fursa kujikwamua kiuchumi. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez, Mkurugenzi wa Fursa, Ruge Mutahaba na Kiongozi wa Shirika la Maendeleo ya Jamii na Ubunifu Endelevu (HDIF),David McGinty.
,Mkurugenzi wa Fursa, Ruge Mutahaba akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habarai jijini pichani kati ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji,Bengi Issa 

Baraza la Taifa la Uwezeshaji, Umoja wa Mataifa (UN) na shirika la Human Development Innovation Fund (HDIF) leo wameungana na kuzindua mafunzo ya aina tano za ujuzi kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata mbinu bora za ujasiriamali mdogo na wa kati hapa nchini Tanzania. 

Misingi ya ujuzi na mbinu hizi inalenga kukuza na kuboresha uzoefu wa vijana katika ujasiriamali. Ujuzi huu utawasaidia kuwa imara na kuweza kuhimili ushindani wa kiuchumi. 

Mafunzo haya yenye mbinu tano yatalenga ukuzaji wa bidhaa, mauzo, kumbu kumbu za mauzo, ujuzi wa kawaida pamoja na taratibu na sheria za kufanya kazi. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji, Bw. Beng’i Issa alisema anaamini ya kwamba uzinduzi wa mafunzo haya yatasaidia Taifa kufanikisha malengo ya kuwa nchi ya viwanda ifikapo 2015. 

Kuendeleza wajasiriamali ni muhimu sana kama kweli Tanzania ina lengo la kuwa nchi ya viwanda. Wajasiriamali watajenga fursa nyingi ambazo zitatoa ajira kwa watanzania na kuinua uchumi wa nchi. "Uzinduzi wa mafunzo ya mbinu tano za kukuza ujasiriamali ni njia mojawapo sahihi itakayoleta mafanikio katika Taifa letu", alisema Issa. 

"Kigezo kikubwa kinachohitajika kuwa mshiriki wa mafunzo hayo ni kuwa na ujuzi wa ujasiriamali na kuwa na malengo endelevu ya kukua kibiashara", alisema Issa. 

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez alisema ni muhimu kwa taifa lolote lenye nia ya kujiendeleza kufikia kuwa nchi ya viwanda halina budi kuwathamini na kuwaendeleza wajasiriamali wadogo na wa kati. Bw. Rodriguea alisisitiza kuwa wajasiriliamali ndio wenye nafasi kubwa ya kutoa ajira pamoja na kukuza uchumi wa nchi. 

Naye mwanzilishi wa Taasisi ya Fursa Tanzania, Bw. Ruge Mutahaba alisema uzinduzi wa mafunzo ya mbinu tano za kukua kijisiriamali kutafungua nafasi pana kwa taasisi na watu binafsi watakaotaka kuunga mkono na kuwa sehemu ya kuendeleza mradi huu. Hii itawapa nafasi pekee ya kushirikiana na vijana wajisiriliamali kutatua changamoto zinazowakabili katika kufikia malengo yao.

MAOFISA UGANI WATAKIWA KUWA NA MASHAMBA YA MFANO

 Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus (kulia), akitoa mada katika mafunzo ya kilimo ya siku moja kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bushosa, Sengerema mkoani Mwanza leo hii ambayo yameratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa hilo. 
 Mtaalamu wa magonjwa ya pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Stella Chirimi akitoa mada katika mafunzo hayo.
 Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon akizungumza katika mafunzo hayo.
 Ofisa Ugani kutoka Kata ya Luharanyogu, Aminiel John, akichangia mada.
 Ofisa Ushirika wa Wilaya ya Buchosa, Nyabange Theopista akichangia jambo kwenye mkutano huo.

MAGAZETI YA TANZANIA LEO MAY 23,2017


Magazeti zaidi>Bofya Hapa

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM-BARA PHILIP MANGULA AKUTANA NA MKURUGENZI WA NDI KANDA YA MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA

May 22, 2017

 Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Phili Mangula akikmkaribisha Mkurugenzi wa Tasisi ya Kimarekani inayoshughulikia masuala ya Demokrasia Duniani (NDI), Kanda ya Mashariki na Kusini Mwa Afrika, Dk. Keith Jennings, kwa ajili ya mazungumzo, Ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga. na katikati na Maofisa Waandamizi wa Taasisi hiyo.
 Mkurugenzi wa Tasisi ya Kimarekani inayoshughulikia masuala ya Demokrasia Duniani (NDI), Kanda ya Mashariki na Kusini Mwa Afrika, Dk. Keith Jennings akisaini kitabu cha wageni
 Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula akizungumza na Mkurugenzi wa Tasisi ya Kimarekani inayoshughulikia masuala ya Demokrasia Duniani (NDI), Kanda ya Mashariki na Kusini Mwa Afrika, Dk. Keith Jennings
 Mkurugenzi wa Tasisi ya Kimarekani inayoshughulikia masuala ya Demokrasia Duniani (NDI), Kanda ya Mashariki na Kusini Mwa Afrika, Dk. Keith Jennings akimfafanulia jambo, Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula wakati wa mazungumzo hayo
 Mazungumzo yakiendelea
 Mazungumzo yakiendelea
 Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara PhilipMangula akifafanua jambo
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akiteta jambo na Ofisa mipango mkazi wa NDI, Nahija Dodd wakati wa mazungumzo hayo 
 Mkurugenzi wa Tasisi ya Kimarekani inayoshughulikia masuala ya Demokrasia Duniani (NDI), Kanda ya Mashariki na Kusini Mwa Afrika, Dk. Keith Jennings akimfafanulia Mzee Mangula moja ya kazi za NDI
 Mkurugenzi wa Tasisi ya Kimarekani inayoshughulikia masuala ya Demokrasia Duniani (NDI), Kanda ya Mashariki na Kusini Mwa Afrika, Dk. Keith Jennings akimuaga Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula, baada ya mazungumzo yao.
 Wakifurahi baada ya mazungumzo
 Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara akimuaga Mahija
 Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara- Philip Mangula akiagana na Mkurugenzi Mkazi wa NDI Sandy Quimbaya baada ya mazungumzo
 Ugeni ukiondoka
 Ugenni ukiondoka
Mama Chintika akiuaga ugeni wakati ukiondo. Picha na Bashir Nkoromo

ASKARI WA JESHI LA POLISI KATIKA AJALI USO KWA USO DAR ES SALAAM

Askari wa Jeshi la Polisi  wakipima ajali iliyohusishwa na  Gari lenye namba za Usajili  namba T 757 BNS na T 876 DEJ iliyotokea jana jioni eneo la  Ngoroka  Kata ya Towangoma Mkoa wa Dar es Salaa jana jioni baada ya mwenyegari lenye namba za usajili T 757 BNS kutaka kuyapita magati yaliyokuwa mbele yake na kujikuta anashindwa kurudi upande wake wa kushoto wakati alipokuwa akitokea upande wa Kongowe akiwa katika mwendo wa kasi na mwenye gari lenye namaba za usajili  T 876 DEJ akitokoa upande wa Kigamboni, Dereva wa  Gari lenye namba za Usajili  namba T 757 BNS inasemekana alikimbia na kulitelekeza gari hili na majeruhi mmoja kukimbizwa Hospitali. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

 

 Mmoja wa majeruhi akiwa hajitambui katika Gali lenye nama za usajili, T 863 CEH  ambapo ametowa msaada wa kumuwahisha Hospitali majeruhi huyo
 Dereva wa gari lenye namba za usajili T 876 DEJ akitowa maelezo kwa Askari wa Usalama barabaraniMARY BUJIKU KATIKA MAHAFALI YA TAHLISO YA WAHITIMU BORA WA VYUO VIKUU NCHINI

Mary Bujiku ni miongoni mwa wahitimu 120 waliofanya vizuri sana, katika mitihani yao ya kumaliza masomo katika vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini, ambao kutokana na umuhimu wao Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), liliwaandalia mahafali jijini Dar es Salaam, kwa udamini mkubwa wa PSPF. Pichani, Mary Bujiku akionyesha kuwa mwenye furaha wakati wa mahafali hayo juzi. Tafadahli endelea kuona picha kem kem za mahafali hayo. (pcha zote na Bashir Nkoromo)

ยช