.

UWT YAPULIZA KIPYENGA CHA KUCHUKUA FOMU KUOMBA UONGOZI, YAMUUNGA MKONO JPM KUHUSU MIMBA SHULENI

Jun 30, 2017


NA BASHIR NKOROMO, DAR
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Amina Makilagi leo ametangaza rami tarehe ya Wanachama wa Jumuia hiyo kuanza kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi tangu ngazi ya Kata hadi Taifa, na kusema fomu zinatolewa bure, huku akionya kuwa atakayejaribu kutumia rushwa kuomba nafasi yoyote atakatwa.

Pia ametumia ameaema UWT inaunga mkono tamko la Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Magufuli alilolitoa hvi kribuni kwamba, ni marufuku kwa msichana atakayepata ujauzito akiwa shuleni katika mfumo rasmi kurudi masomoni katika mfumo huo rasmi.

Makilangi amesema, UWT inaunga mkono tamko hilo kwa sababu ndiyo maelekezo yaliyomo katika Ilaniya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020, na pia ndiyo Sera ya Serikali katika kusimamia utoaji elimu katika mfumo rasmi hapa nchini.

"Tafiti mbalimbali za Jumuia na Taasisi nyingine hapa nchini na za Kimataifa likiwemo Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataida (UNICEF), Mwanafunzi mjamzito au aliyejifungua ni vigumu kuendelea na masomo katika mfumo ambao umeandaliwa kulingana na Saikolojia ya akili ya mtoto asiye na majukumu ya malezi na ndiyo maana upomfumo uliopendekezwa na sera na ilani ya CCM kwamba anayekatiza masomo katika mfumo rasmi anaweza kuendelea katika mfumo usio rasmi, Mifumo isyo rasmi kwa ajili ya wanafunzi wa aina hiyo na wengine waliokosa masomo katika mfumo wa kawaida ni  kama MEMKWA na QT" , alisema Makilagi.

Alisema UWT inatambua na kuheshimu mapendekezo  ya tafiti hizo kuhusu watoto na pia inakubaliana na sera ya Serikali na Ilani ya CCM kuweka utaratibu bora na wenye manufaa  zaidi wa kuwazuia wajawazito na wazazi  kuendelea na masomo katika mfumo rasmi na badala yake kutengeneza mfumo mbadala wa kupata elimu kwa kuwa kufanya hivyo kumaimarisha nidhamu, na uwezo wa kitaaluma wa watoto.

"Pia UWT inawapongeza Wabunge kwa kupitisha sheria kali kwa wale watakaobainika kusababisha upatikanaji wamimba  kwa wanafunzi, kutetea na kufanikisha ndo za utotoni.  Sheria ya maraekebisho ya sheria mbalimbali namba 2 ya mwaka 2016 ilyofanyiwa marekebisho ya sheria ya elimu ya Sura 353 inaweka wazi dhamira ya Serikali ya kumlinda mtoto wa kike na kutoa onyo kali kwa wale wenye tabia za kuwarubuni na kuwasababishaia mimba zisizotarajiwa  na za utotoni",

"pamoja nakuunga mkono kauli ya Mheshimiwa Rais, pia UWT inawashauri na kuwaomba Wazazi , Walezi na Jamii kwa ujumla, kuwalinda watoto wa kike na kutoa elimu ya kutosha kuhusu masuala ya jinsia, athari za mimba za utotoni na athari za maambukizi ya magonjwa ya zinaa ukiwemo Ukimwi", alisema Makilagi.

UWT imetoa mwito kwa wasichana waliopo shuleni kujizatiti kwenye masomo na kujiepusha na vishawishi kwa kuwa dira ya Tanzania ni kuwa na Taifa lenye uwiano na fursa sawa baina ya wanaume na wanawake hivyo mwito ni kwamba wasichana wajitahidi zaidi ili kulifikia lengo la kuwa washiriki katika ujenzi wa Taifa.

UFUATAYO NI TAARIFA KAMILI KUHUSU UCHAGUZI WA KATIKA UWT

TAARIFA KWA WANACHAMA WA UWT/CCM KUPITIA VYOMBO VYA HABARI – TAREHE 30/06/2017

Mwaka 2017 ni mwaka wa Uchaguzi wa Viongozi ndani Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake ambazo ni Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT), UVCCM na WAZAZI kuanzia ngazi ya Tawi hadi Taifa.

UCHAGUZI WA MATAWI
Kwa upande wa UWT Uchaguzi wa Viongozi ngazi ya Matawi, Matawi yaliyofanya Uchaguzi ni 19,927 sawa na 87% na Matawi ambayo bado kufanya Uchaguzi ni 3,118 sawa na 13%.

UCHAGUZI NGAZI YA KATA/WADI
Tarehe 04/06/2017 hadi tarehe 11/06/2017 tulitoa na kupokea fomu za wanachama walioomba kuteuliwa kuwa Viongozi wa UWT ngazi ya Kata/Wadi. Hatua inayoendelea hivi sasa ni mchakato wa vikao kwa mujibu wa Katiba ya UWT. Uchaguzi wa Kata/Wadi utafanyika kati ya tarehe 25/07/2017 hadi tarehe 28/07/2017.

UCHAGUZI NGAZI YA JIMBO
Tarehe 29/06/2017 hadi tarehe 04/07/2017 kutoa na kupokea fomu na Uchaguzi wa Viongozi wa UWT ngazi ya Jimbo unatarajiwa kufanyika kati ya tarehe 25 – 26/08/2017.


UCHAGUZI WA VIONGOZI WA WILAYA, MKOA NA TAIFA
Tarehe 02/07/2017 hadi 10/07/2017 tutaanza kutoa na kupokea fomu za wanachama wanaoomba kuteuliwa kugombea Uongozi wa Wilaya, Mkoa na Taifa.Utaratibu wa Fomu
Fomu za kugombea Uongozi wa UWT wa Wilaya, Mkoa na Taifa zinapatikana katika Ofisi za UWT Wilaya zote na Mikoa.

Nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti
Fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti UWT, zitatolewa katika Vituo vitatu.

1.       Ofisi ya UWT Makao Makuu Dodoma;
2.       Ofisi Ndogo ya UWT Dar es Salaam;
3.       Afisi Kuu ya UWT Zanzibar;

Nafasi zingine za Kitaifa

1.     Nafasi tano (5) za Halmashauri Kuu ya Taifa, nafasi tatu (3) Bara na nafasi mbili (2) Zanzibar.

2.     Nafasi kumi (10) za Baraza Kuu la UWT, nafasi tano (5) Bara nafasi tano (5) Zanzibar.

3.     Nafasi ya Uwakilishi wa UWT kwenda Jumuiya ya Vijana nafasi moja (1) na nafasi moja ya Mjumbe mmoja kuiwakilisha UWT Wazazi.

4.     Fomu za kugombea nafasi hizo zitapatikana katika Ofisi ya UWT Wilaya na Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar.

5.     MIKUTANO MIKUU YA WILAYA, MIKOA NA TAIFA

(1)       Mikutano Mikuu ya UWT ngazi ya Wilaya itafanyika tarehe kati ya tarehe 21 – 22/09/2017.

(2)        Mikutano Mikuu ya UWT ngazi ya Mikoa itafanyika tarehe kati ya tarehe 25 – 26/10/2017.

(3)       Mkutano Mkuu wa UWT ngazi ya Taifa utafanyika tarehe 01 – 03/11/2017.GHARAMA ZA FOMU
Fomu zote za kugombea Uongozi wa Tawi hadi Taifa zitatolewa bila malipo yoyote.

WITO KWA WANACHAMA
Nitumie nafasi hii kupitia Vyombo vya Habari kuhamasisha wanachama wote wa UWT/CCM wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali ndani ya UWT kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa ifikapo tarehe 02 – 10/07/2017.


ANGALIZO KWA WATENDAJI/VIONGOZI NA WANACHAMA
Mipango ya kutafuta fedha kwa ajili ya gharama za Mikutano ya Wilaya, Mikoa na Taifa iendelee bila kuhusisha uchukuaji wa fomu na kugombea Uongozi ndani ya UWT.

KUZINGATIA KANUNI YA UCHAGUZI
Aidha, ninasisitiza umuhimu wa kuzingatia Katiba na Kanuni ya Uchaguzi wa UWT na Kanuni ya Uchaguzi ya Maadili ya Viongozi wa CCM, lengo ni kuhakikisha Uchaguzi kwa ngazi zote unakuwa Huru na Haki kwa wanachama wote wa UWT/CCM.


RUSHWA
Uchaguzi wa 2017 tunahitaji kupata Viongozi wasiotoa Rushwa  kwa wanachama na wajumbe wasiopokea wala kutoa Rushwa. Lengo ni kupata Viongozi waadilifu na wachapa kazi na wenye moyo wa kufanya kazi za UWT bila kutanguliza maslahi yao binafsi.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

 Imetolewa na:
Ndugu Amina Nassor Makillagi (MNEC, MB)
KATIBU MKUU WA UWT
  30/06/2017 

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NORWAY BORGE BRENDE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha  na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende wanne kutoka (kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga wanne kutoka (kulia)pamoja na vingozi wengine wa Tanzania na Norway mara baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwatazama Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende wakati akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

MAGAZETI YA NDANI NA NJE YA TANZANIA LEO JUNE 30,2017


Magazeti zaidi>Bofya Hapa

POLEPOLE AKUTANA NA VIONGOZI WA CCM TAWI LA UINGEREZA, LEO

Jun 29, 2017

  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza (UK), Kangoma Kapinga, alipowasili ukumbini kwa ajili ya mazungumzo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Katibu wa CCM wa tawi hilo Leybab Mdegela.  
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akisalimiana na Katibu wa CCM Tawi la Uingereza (UK) Leybab Mdegela, alipowasili ukumbini kwa ajili ya mazungumzo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza (UK), Kangoma Kapinga. 
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akienda kuketi kitini tayari kwa mazungumzo na ugeni huo, Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza (UK), Kangoma Kapinga, na Kulia ni Katibu wa CCM wa tawi hilo Leybab Mdegela.  
 Wakiwa tayari kwa mazungumzo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza (UK), Kangoma Kapinga, wakati wa mazungumzo yao Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Katibu wa CCM wa tawi hilo Leybab Mdegela.  
Katibu wa CCM wa tawi hilo Leybab Mdegela (kulia) akifafanua jambo katika mazungumzo hayo. 
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza (UK), Kangoma Kapinga, wakati wa mazungumzo yao Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Wapili kushoto ni Katibu wa CCM wa tawi hilo Leybab Mdegela. 
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akieleza jambo wakati wa mazungumzo yao Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akimfafanulia jambo Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza (UK), Kangoma Kapinga, wakati wa mazungumzo yao Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Katibu wa CCM wa tawi hilo Leybab Mdegela. PICHA: BASHIR NKOROMO

CCM YAOMBOLEZA KIFO CHA RAIS MSTAAFU WA BOTWANA KETUMIRE MASIRE


CCM YARIDHISHWA NA UCHAPAKAZI WA SERIKALI YA JPM KATIKA KUTEKELEZA ILANI

NA BASHIR NKOROMO
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinaridhishwa sana na kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli kwa kuwa serikali hiyo imejikita ipaswavyo katika kutekeleza ilani ya Chama ikiwemo kuipeleka Tanzania katika nchi ya Uchumi wa Viwanda.

Akizungumza na Waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, amesema, CCM imefikia hatua ya kutoa tamko rasmi la kuridhishwa kwake na utendaji kazi wa Serikali hiyo, baada ya Chama kufanya ziara ya uhakiki wa hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa viwanda vikubwa, vya kati na vidogo katika mkoa wa Pwani.

Hivi karibuni CCM ilipata fursa ya kushiriki katika ziara ya Rais Dk. John Magufuli katika mkoa huo wa Pwani, kwa kuwakilishwa na Polepole, ambapo katika ziara hiyo ya siku tatu, Rais alitembelea na kuzindua viwanda kadhaa ambavyo vinaonyesha kuwa vitachangia kwa kasi kuleta mahuisha matumaini ya lengo la Tanzania kuwa nchi ya Uchumi wa Viwanda.

"Katika kipindi cha miaka miwili cha Uongozi Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli, mkoa wa Pwani pekee, umeweza kuwa na viwanda vikubwa, vya kati na vidogo zaidi ya 370, hii ni hatua kubwa sana inayoonyesha kuwa Serikali hii imedhamiria kuifikisha Tanzania katika Uchumi wa Viwanda", alisema Polepole.

Polepole amesema, kufuatia uhakiki iliofanya CCM  katika hivyo viwanda zaidi ya 370, viwanda 87 ni vikubwa ambavyo vina uwezo wa uzalishaji bidhaa hadi za kwenda nje ya nchi na kwenda katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba viwanda hivyo vilivyopo mkoa wa Pwani baadhi vimejengwa kwa ubia wa serikali na wadau na vingine wadau wenyewe.

Alisema, miongoni mwa viwanda vilivyoivutia CCM ni kile cha dawa za kuua viluwiluwi vya mbu ambacho ndicho pekee kilichopo Bara la Afrika na kwamba kiwanda hicho kimejengwa kwa ubia wa Serikali ya Tanzania ya Cuba. "Lakini cha kufurahisha zaidi ni kwamba Mheshimiwa Rais Dk.Magufuli ameshanunua lita 100,000 za dawa hiyo ambayo itasambazwa katika maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kupambana na malaria", alisema Polepole.

Polepole alisema, kiwanda kingine ni cha kutengeneza Nondo kilichopo Mlandizi Kibaha, ambacho alisema, kina uwezo wa kuzalisha tani 1000 za nondo kwa siku, na kina uwezo wa kutengeneza mataruma ya reli kwa kutumia malighafi za hapa nchini.

Kiwanda kingine alikitaja kuwa ni cha kuchakata matunda kilichopo Msoga, ambacho alisema, kina uwezo wa kuchakata tani 30 za matunda kwa siku, na kueleza kwamba uwepo wa kiwanda hiki utasaidia sana kuinua uchumi wa wakulima wa matunda katika mkoa wa Pwani, na kwa kutambua hivyo CCM imewaelekeza viongozi kuhakikisha maofisa ugani  wanafika kwa wakulima kutoa elimu ya kilimo cha zao hilo, ili usije kutokea uhaba za matunda kiwanda kitakapoanza kuzalisha.

Polepole alisema, kwa kuzingatia kuwa umadhubuti wa viwanda unaendana pia na Kilimo, CCM imefurahi kuona kuwa imejengwa karakana na  kuunga matrekta na kwamba hadi sasa inamalizia matrekta 140 ambayo alisema, yatauzwa kwa bei nafuu kwa kuwa yanaunganishwa hapa nchini.

Alisema, katika awamu ya pili Karakana  hiyo ambayo imejengwa kwa ubia kati ya Tanzania na  Uholanzi, mitambo itahamishiwa katika eneo la Tamco, Kibaha na badaa ya kuunganisha tu itakuwa ni kiwanda cha kutengenezea hapa nchini matrekta na pia kitakuwa kikiunganisha mabasi aina ya TATA.

UCHAGUZI NDANI YA CHAMA
Akizungumzia Uchaguzi ndani ya Chama, Polepole alisema, Chaguzi za Mashina zimeshakamilika nchini kote kwa asilimia 95, huku akiwataka Wanachama wa CCM wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi za Jumuia na Kata huku akisisitiza kuwa fomu hizo zinatolewa bure.

"Wewe ukijisikia kuwa ni Mwanachama ambaye kwa dhati ya moyo wako unakerwa na shida za wananchi, unajiheshimu, ni mnyenyekevu lakini mkali dhidi ya maovu kachukue fomu kuombe ridhaa ya kugombea nafasi unayotaka", alisema Polepole.

Alisema, fomu katika ngazi za Jumuia na  Kata zimeanza kutolewa tangu Juni 20, mwaka huu, na bdo zinaendelea kutolewa hadi mwezi ujao.

PONGEZI KWA JPM
Kadhalika, Polepole alisema CCM inaipongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Magufuli kwa Ujenzi wa Bwawa la kufua umeme katika mto Rufiji na kwamba hiyo ni hatua muhimu kwa kuwa inaendana na lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Uchumi wa viwanda kwa sababu umeme ndiyo kichocheo kikubwa cha viwanda.

Pia CCM imempongeza Rais Dk. John Magufuli kwa Serikali yake kupeleka miswada Bungeni kwa minajili ya kurekebisha sheria kuhusiana na ulinzi wa madini na maliasili za nchi.

KUTOREJEA MASOMONI BAADA YA KUJIFUNGUA
Akizungumzia kuhusu kauli aliyotoa hivi karibuni Rais Dk. John Magufuli kutoruhusu Wanafunzi kutorejea katika utaratibu wa kawaida wa masomo shuleni, Polepole alisema, CCM inampongeza Rais kwa kauli hiyo na inamuunga mkono kwa dhati kabisa.

"Mnajua baada ya Rais kutoa kauli hii, kuna baadhi ya watu wanajaribu kupotosha, ukweli ni kwamba Rais yupo sahihi na sisi CCM tunamuunga mkono. Mnajua utaratibu na ni kwamba mtoto anapopelekwa shuleni anaanza masomo katika mfumo rasmi, sasa anapopata ujauzito na kwenda kujifungua, haiwezekani tena kurejea masomoni katika mfumo huo. Lakini Siyo kwamba mfumo huo ndiyo wa mwisho, akipenda kuendendelea na masomo ipo mifumo mingine nje ya mfumo rasmi ambayo anaweza akasoma", alisema.

MAGAZETI YA NDANI NA NJE YA TANZANIA LEO JUNE 29,2017


Magazeti zaidi>Bofya Hapa

MTOTO WA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ANG'ARA MAREKANI

Jun 28, 2017

Rashid Jakaya Kikwete(Katikat) ambaye ni mtoto wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, ameg'ara kwa kujinyakulia medali ya dhahabu katika mashindano ya Uwezo wa Kitaaluma yajulikanayo kama GENIUS OLYMPIAD yaliyofanyika nchini Marekani.

Katika mashindano hayo yaliyoshirikisha nchini 63 Duniani, Rashid amejipatia medali hiyo sambamba na wanafunzi wenzake wa Shule ya Sekondari ya Feza Boys ya Dar es Salaam, ambao ni Abdulrazak Juma Mkamia na Abdallah Rubeya

KANALI LUBINGA AFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA CCM TAWI LA UINGEREZA (UK), LEO

 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akimkaribisha Ofisini kwake, Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza (UK), Kangoma Kapinga, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Mwenyekiti huyo ambaye alifuatana na Katibu wa CCM wa tawi hilo Leybab Mdegela alifanya mazungumzo na Kanali Lubinga ikiwemo haja ya kuimarishwa matawi ya CCM yaliyopo nchi za nje.  
 Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza Kangoma Kapinga akisaini kitabu cha wageni Ofisini kwa Kanali Ngemela (katikati), kabla ya mazungumzo yao kuanza. Kushoto ni Katibu wa CCM Tawi la Uingereza Leybab Mdegela.
 Katibu wa CCM Tawi la Uingereza Lebab Mdegela akisaini Kitabu cha wageni. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza Kangoma Kapinga na Katikati ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.
 Katibu wa CCM Tawi la Uingereza Lebab Mdegela akisaini Kitabu cha wageni. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza Kangoma Kapinga na Katikati ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akifafanua jambo wakati akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza Kangoma Kapinga (kulia), katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Katibu wa CCM wa tawi hilo Laybab Mdegela. PICHA: BASHIR NKOROMO-CCM Blog.

MASALIA YA MIJUSI MIKUBWA KUTORUDISHWA NCHINI

NA OCTAVIAN KIMARIO-WHUSM DODOMA
Wazo la kuwarudisha nchini Dinosaria halina tija kutokana na ugumu wa Kiteknolojia na gharama ikilinganishwa na faida za kuchukua hatua hiyo.

Akijibu swali la Mbunge wa Mchinga Hamidu Hassan Bobali aliyetaka kujua kauli ya mwisho ya Serikali kuhusu faida ambayo wananchi wa Lindi na Tanzania kwa ujumla wananufaika kutokana na mabaki hayo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Ramo Makani amesema Tanzania itaendelea kusisitiza kupata manufaa kutokana na uwepo wa Dinosaria wake huko Berlin-Ujererumani.

“Kufuatia majadiliano ya kina yaliyohusisha wataalamu wabobezi katika masuala ya Malikale kutoka pande zote mbili imekubalika kuwa Serikali ya Ujerumani itaendesha shughuli za utafiti zaidi huko Tendaguru na katika maeneo jirani ili kuwezesha uchimbaji wa mabaki ya Dinosaria wengine yanayoaminika kuwepo katika maeneo hayo pamoja na kuanzisha Kituo cha Makumbusho ili shughuli za Utalii zifanyike katika eneo hilo na kuvutia watalii kutoka nchini na nje ya nchi” alisisitiza Mhe. Makani.

Kuhusu Serikali kupunjwa mapato yatokanayo na viingilio katika Makumbusho ya Elimu Viumbe ya Berlin, Mhandisi Makani amesema jambo hilo halina ukweli wowote kwani ni ngumu kufahamu ni kiasi gani hupatikana kama kiingilio kuwaona Mijusi kutoka Tanzania kwakuwa Makumbusho hiyo ina kumbi nyingi zenye masalia kutoka nchi mbali mbali za Afrika na gharama za kuendesha Makumbusho hiyo hutolewa na Serikali ya Ujerumani.

Ameeleza kuwa Serikali ya Ujerumani itafadhili zoezi la uimarishaji idara inayohusika na Malikale katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwezesha upatikanaji wa wataalamu wa kutosha wa fani husika ilikuendeleza Utalii wa Malikale nchini.

Mijusi mikubwa (Dinosaria) ilichimbwa katika Kilima cha Tendaguru,mkoani Lindi kati ya waka 1909 na mwaka 1913 na kupelekwa katika makumbusho ya Elimu Viumbe ya Berlin nchini Ujerumani.

MAGAZETI YA NDANI NA NJE YA TANZANIA LEO JUNE 28,2017


Magazeti zaidi>Bofya Hapa

RAIS MSTAAFU ALHAJI ALI HASSAN MWINYI AONGOZA SWALA YA EID EL FITR JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Jun 26, 2017

Rais mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi akitoa Salamu za Eid el Fitr kwa waislam baada ya Swala ya Eid el Fitr katika viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam, leo Juni 26, 2017
Pichani kulia ni Rais mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi sambamba na waumini wengine wakiswali swala ya sikukuu ya Eid El Fitr iliyofanyika mapema leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja,jijini Dar es Salaam.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Al Had Mussa Salum akitoa mawaidha yake wakati wa Swala ya Eid El Fitr katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Waumini wa dini ya Kiislamu wakifuatilia mawaidha mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa katika Swala ya Eid El Fitr,iliyofanyika kwenye viwanja vya mnazi mmoja mapema,leo jijini Dar es Salaam
  Waumini wa dini ya Kiislamu wakifuatilia mawaidha mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa katika Swala ya Eid El Fitr,iliyofanyika kwenye viwanja vya mnazi mmoja mapema,leo jijini Dar
  Waumini wa dini ya Kiislamu wakifuatilia mawaidha mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa katika Swala ya Eid El Fitr,iliyofanyika kwenye viwanja vya mnazi mmoja mapema,leo jijini Dar esSalaam 


 
 
 
  Waumini wa dini ya Kiislamu wakiswali swala ya Eid El Fitr,katika viwanja vya mnazi mmoja mapema,leo jijini Dar es Salaam.
   Waumini wa dini ya Kiislamu wakijumuika pamoja katika swala ya Eid El Fitr,katika viwanja vya mnazi mmoja mapema,leo jijini Dar es Salaam
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Dkt Hussein Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mhe.Salum Hapi mara baada ya kuwasili katika Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika mapema leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,Pichani kati ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Al Had Mussa Salum .
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mhe.Salum Hapi mara baada ya kuwasili katika Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika mapema leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Pichani kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha CUF,Prof Haroun Lipumba na waumini wengine wakiwasili katika viwanja vya Mnazi mmoja kwa ajili ya kushiriki swala ya Eid El Fitr jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim akiongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Al Had Mussa Salum pamoja na Mkuu wa Wilaya ya  Kinondoni,Mhe.Salum Hapi kushiriki kwenye swala ya sikukuu ya
Eid El Fitr iliyofanyika mapema leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja,jijini Dar es Salaam. 
ยช