.

NGO'S ZAPEWA SOMO KUFANYA KAZI KWA WELED

Jul 28, 2017

IGP SIRRO AWAFAGILIA POLISI MKOA WA SINGIDA

IGP Simon Sirro mjini Singida, leo
NA GASPER ANDREW, SINGIDA
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amelipongeza jeshi hilo mkoani Singida kwa juhudi za kupunguza matukio ya uhalifu yakiwemo ya utekaji wa magari kwa kiwango kikumbwa.

IGP  Siro ametoa pongezi hizo  leo asubuhi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  kweye viwanja vya kambi  ya kikosi  cha kuzuia fujo (FFU) mjini  hapa.

Amesema matukio ya uhalifu mbalimbali mkoani Singida yamekupungua kwa kiwango kikubwa kwa  sasa, ikilinganishwa na miaka ya  nyuma.

“Hatua hii  inachangia  uwepo  wa amani  na utulivu kwa  wananchi  wa  mkoa wa Singida hivyo  kutoa fursa   kuweza  kujiletea maendeleo yao ya mkoa na  taifa   kwa ujumla” amesema.

IGP Siro  amesema  mafanikio  hayo yamechangiwa   na wananchi kwa kiwanngo  kikubwa  kwa kutoa ushuirikiano  kwa jeshi la polisi. 

Akifafanua amesema wananchi wamekuwa wakitoa  taarifa sahihi na kwa  wakati kwa jeshi la polisi  pindi wanapobaini  dalili  ama  matukio ya kihalifu.

“Kwa sasa kwa kweli  wananchi hata ninyi waandishi  wa habari mnatupa  ushirikiano  mzuri sana. Ushirikiano huu unachangia  kazi zetu kuwa nyepesi  na za mafanikio makubwa. Sasa  hivi  kule Kibiti mkoani Pwani, wananchi wanatusaidia mno taarifa  zinazohusu  mauaji ya watu  wasiokuwa  na hatia”, amefafanua zaidi.

IGP Siro amesema kwa sasa Tanzania inaonewa wivu na nchi jirani kwa namna tulivyo dhibiti matukio ya kihalifu na kupelekea nchi kuendelea kudumisha amani na utulivu.

Wakati huo huo, Mkuu huyo  wa jeshi la polisi ametumia fursa hiyo  kuwaomba wananchi  waendelee  kushirikiana na jeshi hilo, kufichua  baadhi ya watu wanaojihusisha na matukio mbalimbali   ya kihalifu ili waweze kuchukulia  hatua stahiki.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro wakati wa paredi ya polisi iliyoandaliwa kwa ajili yake leo kwenye viwanja vya Kambi ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia( FFU) mjini Singida

Mkuu wa Jeshi la Polisi  nchini IGP Simon Sirro akikagua baadhi ya askari wa jeshi la polisi  mjini  Singida leo wakati wa paredi maalum ya ukaguzi iliyoandaliwa kwa ajili yake.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA MAJESHI WA INDIA, LEO

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkaribisha kwa ajili ya mazungumzo Mkuu wa Majeshi wa India, Admiral  Sunil Lanba Ofisini kwake jijini Dar es Salaam, leo Julai 28, 2017. Kulia ni Mkuu wa Majeshi, Jeneral Venance Mabeyo
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Majeshi wa India, Admiral  Sunil Lanba Ofisini kwake jijini Dar es Salaam, leo Julai 28, 2017. Kulia ni Mkuu wa Majeshi, Jeneral Venance Mabeyo
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Majeshi wa India , Admiral Sunil Lanba  (kulia kwake) pamoja na ujumbe wake, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Majeshi, Jeneral Venace Mabeyo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na  Mkuu wa Majeshi wa India Admiral Sunil Lanba  (wapili Kushoto) na Mkuu wa Majeshi nchini, Jeneral Venance Mabeyo (kushoto) baada ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Julai 28, 2017. Kushoto ni Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na  Mkuu wa Majeshi wa India Admiral Sunil Lanba  (wapili Kushoto) na Mkuu wa Majeshi nchini, Jeneral Venance Mabeyo (kushoto) baada ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam, leo Julai 28, 2017. Wapili kushoto ni Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo  na Mkuu wa Majeshi wa India, Admiral  Sunil Lanba (kulia) baada ya mazungumzo yao Ofisini kwa  Waziri Mkuu  jijini Dar es salaam, leo, Julai 28, 2017 . Wapili kulia ni Mkuu wa Majeshi Nchini, Jeneral Venance Mabeyo na kushoto ni Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya.

WASICHANA WAISHUKURU TGGA KUFANIKISHA ZIARA YA MAFUNZO NJE YA NCHI

Wasichana wanachama wa Tanzania Girl Guides wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, wakitokea kwenye ziara ya programu ya miezi sita ya mafunzo ya kubadilisha uzoefu katika masuala ya utamaduni, uongozi na maadili. Kutoka kushoto ni Ummy Mwabondo alikwenda Zambia, Edna Chembele (Zimbabwe), Elizabeth Betha (Madagascar) na Farida Mjoge aliyekuwa Uganda. 

DAR ES SALAAM

Wasichana wanne wanachama wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA) wamerejea nchini kutoka kwenye programu ya mafunzo ya miezi sita katika nchi mbalimbali za Afrika.

Wasichana hao waliokuwa kwenye mafunzo ya kubadilishana uzoefu katika mambo ya utamaduni, uongozi na maadili katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Madagascar na Uganda wameipongeza TGGA kwa kufanikisha ziara hiyo yenye mafanikio makubwa katika maisha yao.


Walipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jana kwa ndege ya Kenya Airways, walilakiwa na Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba, ndugu jamaa na marafiki huku wengine wakivishwa mashada na kupatiwa zawadi mbalimbali. Wasichana waliokwenda kwenye mafunzo hayo ni; Ummy Mwabondo, Elizabeth Betha, Edna Chembele na...

YANGA U20 YAWADUWAZA MBEYA CITY FC WAKIWA KAMILI UWANJA WA SOKOINE MBEYA NA KUTANGULIA FAINALI

 Nahodha wa timu ya Yanga, Ayoub Mohamed 'Pilo' (kulia) akimzunguka Mshambuliaji wa Mbeya City, wakati wa mchezo wa Hisani ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS,  kwa ajili ya kuchangia kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya jana. Katika mchezo huo Yanga U20 iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 na kutinga fainali za mechi hizo. Mchezo wa fainali utachezwa kesho na mshindi kati ya Simba B na Tanzania Prisons wanaocheza leo. 
 Kikosi cah Yanga U20 kilichowaduwaza Mbeya City
 Kikosi cha Mbeya City cha msimu mpya ujao wa ligi.
 Said Mussa, (kulia) akijaribu kuwatoka mabeki wa Mbeya City.
 Wote hewani kuwania mpira
*******************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Mbeya
TIMU ya Vijana ya Yanga U20 jana iliwashangaza mashabiki wa soko waliojitokeza kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na kuacha gumzo baada ya kuwaduwaza Mbeya City wanaoshiriki Ligi Kuu Bara kwa kuwachapa mabao 3-0 katika mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI.
Mechi hizo za Hisani zimeandaliwa na Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS, ambapo zinashirikisha jumla ya timu Nne za Yanga U20 na Simba U20 kutoka jijini Dar es Salaam, huku Mbeya City na Tanzania Prisons zikiwa ni zile zinazoshiriki Ligi Kuu Bara.
Kabla ya mchezo huo kuanza wakati timu zikipasha misuli, mashabiki waliokuwapo uwanjani hapo baadhi walisikika wakijutia kuingia uwanjani kwa kuhisi kukosa burudani, lakini kadri mchezo ulivyokuwa ukiendelea baadhi ya mashabiki walianza kubadilika na kuanza kuwashangilia vijana hao wa Yanga U20, waliokuwa wakionyesha kandanda safi na kuwainua vitini mashabiki wa Soka wa jiji la Mbeya.
Katika mchezo huo uliokuwa wa kuvutia tayari Yanga wametangulia fainali na kusubiri mshindi wa mchezo wa leo kati ya Simba U20 na Tanzania Prisons ambapo fainali hiyo itachezwa siku ya Jumamosikwenye Uwanja wa Sokoine.
Mabao ya Yanga yalifungwa na Maka Edward, katika dakika ya 30 kipindi cha kwanza, akimalizia pasi nzuri ya Said Mussa na dakika ya 64 kipindi cha pili kwa mkwaju wa penati, baada ya kipa wa Mbeya City, Fikirini Bakari, kumchezea rafu mshambuliaji wa Yanga,Paul Godfrey, ndani ya eneo la hatari, huku pazia la mabao likifungwa na Festo Greyson, katika dakika ya 79 baada ya kazi nzuri ya Paul Godfrey, aliyemtoka beki wa kushoto wa Mbeya city na kupiga krosi nzuri iliyozaa bao hilo.
Akizungumzia matokeo hayo Kocha msaidizi wa Mbeya City Mohamed Kijuso, alisema kuwa kwa upande wake amechukulia ni matokeo ya kawaida na kutokana na kwamba hakuna wanachopoteza bali ilikuwa ni kipimo tosha kwa wachezaji wake ambao baadhi ni wageni waliojiunga na timu msimu huu kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu na kuongeza kuwa ameona mapungufu mengi ambayo atayafanyia kazi na Kocha mkuu atakayejiunga na kikosi hicho.
''Kikubwa ni mazoezi kwani tayari nimeona mapungufu ndani ya kikosi changu, nitayafanyia kazi na Kocha atakayejiunga nasi hapo baadaye, ila mashabiki watambue kuwa haya ni matokeo tu ya mchezo na hakuna atulichopoteza kwani ulikuwa ni mchezo wetu wa kwanza kujiandaa na kuangalia kikosi chetu kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu''. alisema Kijuso.
Kwa upande wake Kocha wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, alisema kuwa amefurahishwa na matokeo hayo ambayo alikuwa akiyatarajia baada ya kuona wapinzani wake wamepanga Kikosi cha Ligi Kuu, huku yeye akiwaamini na kuwapa majukumu Vijana wa U20, ambao hawakumuangusha baada ya kufuata maelekezo waliopewa.
''Kwa kweli Vijana wangu wamenifurahisha sana na matokeo haya kwa upande wangu kama mwalimu niliyatarajia na hasa baada ya kuona wapinzani wakiwa na kikosi cha wachezaji wanaoshiriki Ligi Kuu, kwani nilijua watacheza kwa kuwazania vijana wangu na kujiamini sana jambo ambalo vijana wangu walilitumia kuwashangaza na hawakuamini kilichowakuta katika dakika 90 za mchezo,
Mimi nilikuwa na vijana wawili tu walicheza ligi msimu uliopita na mmoja ambaye amepandishwa msimu huu, lakini niliwaamini zaidi vijana na kuwapangia Mhilu tu aliyeshiriki ligi iliyopita ili kuwapa hamasa wenzake jambo ambalo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa'', alisema  Nsajigwa
 Mshambuliaji  wa timu ya Yanga U20, Said Mussa (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Mbeya City, Erick Kyaruzi, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya jana Julai 27, 2017. Katika mchezo huo Yanga U20 walishinda mabao 3-0.
 Mshambuliaji wa timu ya Yanga U20,Yusuph Namiundu, (katikati), akijaribu kuwatoka mabeki wa Mbeya City, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya jana Julai 27, 2017. Katika mchezo huo Yanga U20 walishinda mabao 3-0. 
 Mshambuliaji wa timu ya Yanga U20,Paul Godfrey, (kulia), akimtoka mchezaji wa Mbeya City, Anthony, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya jana Julai 27, 2017. Katika mchezo huo Yanga U20 walishinda mabao 3-0.
 Beki  wa timu ya Yanga U20, Mawazo Gawasa, (kushoto) akiwadhibiti wachezaji wa Mbeya City, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya jana Julai 27, 2017. Katika mchezo huo Yanga U20 walishinda mabao 3-0.
 Beki  wa timu ya Yanga U20, Mawazo Gawasa, (kushoto) akichuana kuwania mpira na mchezaji wa Mbeya City, wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya jana Julai 27, 2017. Katika mchezo huo Yanga U20 walishinda mabao 3-0.
 Beki wa timu ya Yanga U20, Bakari Jomba, (kushoto) akichuana kuwania mpira na mchezaji wa Mbeya City 'Demba Ba', wakati wa mchezo wa Hisani wa kuchangia Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya jana Julai 27, 2017. Katika mchezo huo Yanga U20 walishinda mabao 3-0. Kulia ni Saad Awadh, akijiandaa kutoa msaada.
 Nginja nginja, hapiti mtu hapaaa
 Pilo wa Yanga, akimiliki mpira....
 Yusuph Mhilu, akimzunguka beki wa Mbeya City
 Heka heka langoni mwa Yanga B.....
 Mratibu wa mechi hizo, Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI Tanzania TACAIDS, Elizabeth Kaganda, akizungumz na waandishi wa habari baada ya kumalizka kwa mchezo huo.
 Mratibu msaidizi, Teddy Mapunda, akizungumza na waandishi baada ya kumalizika mchezo huo.
 Krosi murua......
 Said Mussa akimtoka beki wa Mbeya City na kutoa pasi iliyozaa bao la kwanza.
 Wachezaji wa Yanga U20, wakishangilia bao la pili
 Hii ndiyo ilikuwa penatoi iliyozaa bao la pili
 Vumbi lilitimka kwa watu hawa muda wote....
 
 Kocha Msaidizi wa Mbeya City Kijuso akihojiwa na waandishi baada ya mchezo huo
 KOcha wa Yanga Shadrack Nsajigwa akihojiwa na waandishi baada ya mchezo huo.
 Makocha wa Yanga na Mbeya City wakipeana Fair play baada ya mchezo huo.
 Baada ya mchezo huo wachezaji wakizungukwa na mashabiki wao.
Mazoezi kabla ya mchezo huo.
ยช