Breaking News

Your Ad Spot

Jul 28, 2017

IGP SIRRO AWAFAGILIA POLISI MKOA WA SINGIDA

IGP Simon Sirro mjini Singida, leo
NA GASPER ANDREW, SINGIDA
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amelipongeza jeshi hilo mkoani Singida kwa juhudi za kupunguza matukio ya uhalifu yakiwemo ya utekaji wa magari kwa kiwango kikumbwa.

IGP  Siro ametoa pongezi hizo  leo asubuhi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  kweye viwanja vya kambi  ya kikosi  cha kuzuia fujo (FFU) mjini  hapa.

Amesema matukio ya uhalifu mbalimbali mkoani Singida yamekupungua kwa kiwango kikubwa kwa  sasa, ikilinganishwa na miaka ya  nyuma.

“Hatua hii  inachangia  uwepo  wa amani  na utulivu kwa  wananchi  wa  mkoa wa Singida hivyo  kutoa fursa   kuweza  kujiletea maendeleo yao ya mkoa na  taifa   kwa ujumla” amesema.

IGP Siro  amesema  mafanikio  hayo yamechangiwa   na wananchi kwa kiwanngo  kikubwa  kwa kutoa ushuirikiano  kwa jeshi la polisi. 

Akifafanua amesema wananchi wamekuwa wakitoa  taarifa sahihi na kwa  wakati kwa jeshi la polisi  pindi wanapobaini  dalili  ama  matukio ya kihalifu.

“Kwa sasa kwa kweli  wananchi hata ninyi waandishi  wa habari mnatupa  ushirikiano  mzuri sana. Ushirikiano huu unachangia  kazi zetu kuwa nyepesi  na za mafanikio makubwa. Sasa  hivi  kule Kibiti mkoani Pwani, wananchi wanatusaidia mno taarifa  zinazohusu  mauaji ya watu  wasiokuwa  na hatia”, amefafanua zaidi.

IGP Siro amesema kwa sasa Tanzania inaonewa wivu na nchi jirani kwa namna tulivyo dhibiti matukio ya kihalifu na kupelekea nchi kuendelea kudumisha amani na utulivu.

Wakati huo huo, Mkuu huyo  wa jeshi la polisi ametumia fursa hiyo  kuwaomba wananchi  waendelee  kushirikiana na jeshi hilo, kufichua  baadhi ya watu wanaojihusisha na matukio mbalimbali   ya kihalifu ili waweze kuchukulia  hatua stahiki.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro wakati wa paredi ya polisi iliyoandaliwa kwa ajili yake leo kwenye viwanja vya Kambi ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia( FFU) mjini Singida

Mkuu wa Jeshi la Polisi  nchini IGP Simon Sirro akikagua baadhi ya askari wa jeshi la polisi  mjini  Singida leo wakati wa paredi maalum ya ukaguzi iliyoandaliwa kwa ajili yake.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages