.

KUTOKA RADIO UHURU FM- FM - 95.7 FM DAR ES SALAAM

Jul 14, 2017

14-7-2017                                               Pongezi                                           1:00PM
DAR ES SALAAM,        
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imekipongeza Kituo cha Uhuru FM, ambacho kimekuwa kikitoa ushirikiano na msaada wa hali ya juu katika kutekeleza majukumu ya kila siku ya Wizara hiyo.
          Chombo hiki cha Uhuru FM kimekuwa mstari wa mbele katika kutangaza matukio au shughuli za Wizara hiyo kwa kiwango cha hali ya juu hivyo kuchangia na kuwezesha Watanzania na wasio Watanzania kupata taarifa za shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
          Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, CHRISTINA MWANGOSI, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, amesema ushirikiano huo umeiwezesha jamii kuendelea kupata taarifa kwa haraka, hivyo Wizara itaendelea kushirikiana na Uhuru FM kwa hali na mali ili kuiwezesha jamii kupata taarifa muhimu zinazohusu Wizara hiyo.

NG/PN                                                       NET                                                 10

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª