Breaking News

Your Ad Spot

Jul 24, 2017

MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2011-2016 WAKUTANA DODOMA KUJADILI AJENDA YA KILIMO NA USALAMA WA CHAKULA

Mhe. Mary Nagu (Mb), Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Kilimo, Mifugo na Uvuvi, ambaye ndiye aliyekuwa Mgeni Rasmi katika Kongamano la Mama shujaa wa Chakula, akifanya ufunguzi wa Kongamano hilo lililofanyika Dodoma.
Bi.Jovitha Mlay, Meneja wa Kampeni kutoka Shirika la Oxfam Tanzania akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la Mama Shujaa wa Chakula linalofanyika mjini  Dodoma. 
Aliyewahi kuwa mshiriki wa shindano la Mama Shujaa wa ChakulaSister Martha Waziri,  akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la Mama Shujaa wa Chakula linalofanyika Dodoma.
Pili kishinje Itamba, aliyewahi kuwa mshiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la Mama Shujaa wa Chakula linalofanyika Dodoma.
Evelyn Kagoma akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la Mama Shujaa wa Chakula linalofanyika Dodoma.
Anna Oloshuro, aliyewahi kuwa mshiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la Mama Shujaa wa Chakula linalofanyika Dodoma.
Shughuli mbalimbali zikiendelea wakati wa ufunguzi wa kongamano la Mama Shujaa wa Chakula linalofanyika Dodoma.
Eluka Kibona kutoka Oxfam akiwasilisha mada wakati wa ufunguzi wa kongamano la Mama Shujaa wa Chakula linalofanyika Dodoma.
Waliowahi kuwa washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula wakifurahia jambo wakati wa ufunguzi wa kongamano la Mama Shujaa wa Chakula linalofanyika Dodoma.
Neema Hilonga(wa katikati) aliyewahi kuwa mshiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa Mhe. Mary Nagu (Mb), ( Kulia) Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge Kilimo, Mifugo na Uvuvi (kulia), Mkurugenzi Mkazi wa shirika la Oxfam Tanzania, Francis Odokorach (Kushoto) wakati wa ufunguzi wa kongamano la Mama Shujaa wa Chakula linalofanyika Dodoma.
Picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa kongamano la Mama Shujaa wa Chakula linalofanyika Dodoma.
Kongamano la Mama Shujaa wa Chakula lenye lengo la kuwakutanisha washiriki wa Mama Shujaa wa Chakula kwa Msimu wa kwanza hadi wa tano(2011-2015) wamekutana mjini Dodoma kwa lengo la kuangalia Ajenda mpya ya Mama shujaa wa Chakula kuhusiana na Kilimo na Usalama wa Chakula.

Akizungumza leo mjini Dodoma Meneja wa Kampeni, Jovitha Mlay alisema hii ni  mara ya kwanza kufanya kongamano hilo ambalo limewakutanisha washiriki  zaidi ya 50 kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania.
Alisema kongamano hilo pia limewakutanisha washiriki hao kama sehemu ya kuangalia na kushawishi serikali katika masuala ya  kisera,kibajeti na kimkakati yanayohusiana na kilimo hususani kwa wanawake wazalishaji  wadogo wa chakula na  wataangalia uzoefu wa washiriki hao waliokutana wakati walivyoshiriki shindano hilo hadi sasa katika suala la kisera na changamoto walizokutana.

“Tumekutana leo kwa lengo la kusisitiza umuhimu wa wazalishaji wadogo wa chakula na kuendelea kusherekea mafanikio waliokuwa nao kwani zaidi ya asilimia 80 ya chakula uzalishwa na wazalishaji wadogo wa chakula,”alisema Devotha
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Kilimo,Mifugo ,Uvuvi na Maji ambae ndio alikuwa mgeni rasmi wa kongamano hilo, Mh. Mary Nagu alisema kuwa umasikini nchini Tanzania  hauwezi kuisha kama wanawake hawataendelea kupambana katika ujasiriamali, kilimo,uvuvi na mifugo .
Nagu alisema wanawake wapo wengi nchini na uwezo wao ni mkubwa katika kukomboa taifa katika kuondokana na  umaskini hivyo ni vema wakasaidiwa na kunyanyuliwa .

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Oxfam nchini ,Francis Odokorach alisema takwimu zinaonyesha kuwa  asilimia 81 ya wanawake nchini Tanzania wamejikita katika kilimo huku wanaume wakiwa asilimia 73.
“Oxfam ni shirika la kimataifa linalofanya kazi katika nchi 90,ikiwemo Tanzania,tunaimani kufanikisha mabadiliko endelevu kwa kuwainua wakulima wanawake wadogo kwa kuwasaidia katika sekta ya kilimo,”alisema Odokorach
Alisema  kutokana na wanawake kuwa na nguvu katika kilimo,Serikali ingewapa kipaumbele wanawake hao katika rasilimari zinazohitajika kwani wao ni miongoni mwa watu wanaochangia pato la taifa.

 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages