.

RAIS AMTEUA PRO. LUOGA KUWA MWENYEKITI MPYA BODI YA WAKURUGENZI TRA

Jul 11, 2017

Rais Dk. John Pombe Magufuli leo tarehe 11 Julai, 2017 amemteua Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (Taaluma), Prof. Florens D.A.M Luoga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Prof. Florens D.A.M Luoga anachukua nafasi ya Bernard Mchomvu ambaye Bodi yake ilivunjwa na uteuzi wake kutenguliwa. Uteuzi wa Prof. Florens D.A.M Luoga unaanza mara moja.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช