Breaking News

Your Ad Spot

Jul 16, 2017

SERIKALI IPO KATIKA HATUA ZA MWISHO KUIDHINISHA BILIONI 1.6 KUTOKA MFUKO WA GEPF KWA AJILI YA KUJENGA KINU CHA KUYEYUSHIA VYUMA KATIKA KIWANDA CHA KMTC

 Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Joakim Mhagama,wa pili kulia  jana alipata fursa ya kutembelea  kiwanda cha kutengeneza vipuri na mashine cha Kilimanjaro Machine Tools Limited (KMTC),wa tatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh.Anna Mghwira na wa kwanza kulia ni Meneja mkuu Kilimanjaro Machine Tools Eng.Adriano Nyaluke akitoa taarifa za uzalishaji wa kiwanda hicho(Picha na Pamela Mollel Arusha)




 Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagama akiteta jambo na wakurugenzi wa mifuko ya jamii jana katika ziara yake katika kiwanda cha kutengeneza vipuri na mashine cha Kilimanjaro Machine Tools Limited (KMTC),Kulia ni Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa GEPF Mh..Daud Msangi ,kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa Pensheni wa PPF Mh. William Erio




 Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa GEPF Mh..Daud Msangiakizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda hicho,alisema mfuko wa hifadhi ya jamii ya GEPF umeshakamilisha mkopo wa bilion 1.6 kwaajili ya kuboresha kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na kutengeneza kinu cha kuyeyushia vyuma,kukarabati mfumo wa umeme,pamoja na kununua maligafi


  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagam akiwa anatoa maelekezo katika kiwanda hicho ambapo alisema kuboreshwa kwa kiwanda hicho kitasaidia ajira kwa vijana


 Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Wizara ya viwanda,Biashara na Uwekezaji Eng.Elli Pallangyo akitoa ufafanuzi kwa Waziri.
  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagam akiangalia baadhi ya vyuma vilivyo zalishwa katika kiwanda hicho




 Kaimu Mkurugenzi mwendeshaji shirikisho la Taifa Maendeleo (NDC)Mh.Ramson Mwilangali akitoa maelezo kwa Waziri jana Mkoani Kilimanjaro
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh.Anna Mghwira akizungumza mara baada ya kutembelea kiwnda hicho amabapo alisema anaunga mkono jitihada za serikali katika kufufua viwnda hapa Nchini
                                                            Mashine za uzalishaji
 Wa kwanza kushoto ni Joseph Mrina Ambaye ni kiongozi mkuu ndani ya kiwanda hicho akiwa Anna Mosha ambaye yeye ni Fundi wa mashine wakionyesha moja ya mashine ya kuranda mbao waliyoitengeneza hivi karibuni
 Wakurugenzi wa Key Media Arusha Sara Keiya na Anna Keiya wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagam jana Mkoani 
Kilimanjaro


                  Moja ya wafanyakazi katika kiwanda hicho akiendelea na uzalishaji
Katibu wa shirikisho la mifuko ya hifadhi ya jamii Nchini (TSSA)Meshach Bandewa akitoa utambulisho kwa Waziri jana .

Serikali ipo katika hatua za mwisho katika kuhidhinisha bilioni 1.6 kutoka katika mfuko wa hifadhi za jamii GEPF kwaajili ya kujenga kinu cha kuyeyushia vyuma katika  kiwanda cha kutengeneza vipuri na mashine cha Kilimanjaro Machine Tools Limited (KMTC)
Akizungumza jana katika kiwanda hicho mara baada ya kutembelea Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagama,alisema kuwa fedha hizo zitatumika kwaajili ya kuboresha kiwanda hicho  kwa lengo la kufufua kwa kuwa kiwanda hicho kinabeba dhana nzima ya maendeleo ya uchumi wa viwanda kwenye nchi ya Tanzania
Alisema kuwa  mfuko wa GEPF baada ya kupokea maagizo kutoka kwa Rais akihimiza Serikali ya viwanda ,wameweza kujiridhisha kuwa wanauwezo wa kuwekeza katika kiwanda hicho cha kutengeneza vipuri na mashine cha Kilimanjaro Machine Tools (KMTC)
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa Pensheni wa GEPF Daud Msangi alisema kuwa katika uwekezaji huo kiwanda hicho kitaweza kujenga kinu cha kuyeyushia vyuma ambayo ndio maligafi yao kubwa ya kuchonga vipuri na mashine mabalimbali
Aidha aliongeza kuwa kiwnda hicho kinakabiliwa na chagamoto ya umeme ambapo pesa hizo zitatumika katika kukarabati mfumo wa umeme katika kiwanda hicho



No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages