Breaking News

Your Ad Spot

Jul 8, 2017

SERIKALI YAREJESHA UTARATIBU WA HATI PUNGUZO ILIYOBORESHWA KWA KUGAWA VYANDARUA VYENYE VIWATILIFU

Serikali imerudisha utaratibu wa kugawa vyandarua vyenye viwatilifu kwa kina mama wajawazito na watoto ambao wanapatiwa chanjo ya surua kupitia vituo vya kutolea huduma za afya ya uzazi na mtoto na utaanza mwezi ujao.

Afisa Muuguzi kutoka Wizara ya Afya Epifania Malingumu amewaambia wajumbe wa mkutano wa uelimishaji juu ya mpango endelevu wa ugawaji vyandarau vyenye viwatilifu vya mda mrefu kuwa kwa sasa vyandarua hivyo havitapatikana katika maduka kama ilivyokuwa kwenye utaratibu wa ‘hati punguzo’ ya zamani.

Malingumu amesema hapo awali vyandarua hivyo vilikuwa vikitolewa kwa mfumo wa hati punguzo ambapo mama mjamzito alikuwa anatakiwa kutafuta maduka ya mawakala wa vyandarua hivyo mara baada ya kupatiwa hati hiyo katika vituo vya kutolea huduma ya afya ya uzazi.

“Utaratibu wa hati punguzo wa zamani ulikwisha muda wake tangu mwaka 2014, kina mama walikuwa wanapata changamoto katika kutafuta mawakala wa vyandarua lakini utaratibu mpya ni kwamba mama mjamzito au mwenye mtoto mchanga atapewa chandarua chenye viwatilifu palepale atakapokuwa katika vituo vya kutolea huduma za afya ya uzazi” amesema.

Ameongeza kuwa mama atapewa chandarua katika hudhurio la kwanza la kliniki ambapo takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 98 ya wajawazito huhudhuria kliniki angalau mara moja pia vyandarua hivyo vitatolewa kwa idadi ya watoto ambao mama atakua amejifungua kwa wakati huo.

Kwa upande wake Mratibu wa zoezi la ugawaji vyandarua nchini Yusufu Mwita amesema vyandarua vyenye viwatilifu ni nyenzo mojawapo ya kupambana na ugonjwa wa maralia endapo kila mwananchi atazingatia kuvitumia kwa ufanisi.

Mwita amesema kwa mkoa wa Singida kumekua na ongezeko la maambukizi ya Ugonjwa wa maralia kutoka asilimia 0.2 mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 5.5 kwa mwaka 2016 licha ya vyandarua 954,644 kugwiwa mkoani hapa kwa mwaka 2016.

Ameongeza kuwa mkakati wa ugawaji vyandarua umelenga kuwafikia asilimia 85 ya watanzania wote ifikapo 2025 na kuutokomeza ugonjwa wa maralia kwa kushirikisha mbinu mbalimbali ikiwemo kupulizia dawa ya ukoka ili kuthibiti mazalia ya mbu pamoja na kuhakikisha matibabu sahihi ya ugonjwa wa maralia yanatolewa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi amesema Maralia inakuwepo kutokana na kwamba Mkoa wa Singida sio kame una maji ya kutosha hivyo kusababisha mbu kuzaliana kwa wingi.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk. Nchimbi amesema mikakati iliyopo ni mizuri ila inatakiwa iende sambamba na mikakati mingine ya kupambana na ugonjwa wa maralia kwa kuwa ni ugonjwa ambao hupoteza nguvu kazi ya taifa

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages