Breaking News

Your Ad Spot

Aug 10, 2017

AIRTEL YATOA VITABU VYA SAYANSI KWA SEKONDARI SUMBAWANGA

Mwalimu wa masomo ya Kemia katika shule ya sekondari ya Mwazye Sumbawanga, Aidan Mwaibabu (kushoto) akikabidhiwa vitabu mbalimbali vya masomo hayo ya kemia na Mbunge wa Jimbo la Kalambo Josephat Kadege (kulia), jana. Katikati ni  Meneja wa Airtel mikoa ya Katavi na Rukwa.
NA MWANDISHI MAALUM
Ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha kila mtoto kuanzia chekechekea mpaka kidato cha nne wanapata elimu bure, kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania leo imetoa vitabu vya sayansi kwa shule za mkoa wa Sumbawanga vyenye thamani ya shilingi milioni kumi TZS 10,000,000.


Vitabu hivyo vimepokelewa na Mbunge wa Jimbo la kalambo Mh, Josephat Kandege na kugaiwa kwa shule zenye uhabu wa vitabu jimboni humo.


 Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu, Mbunge wa Jimbo la kalambo Mh, Josephat Kandege alisema “ muhimu kutambua mchango wa makampuni binafsi kama Airtel Tanzania kwa juhudi za dhati za kuunga mkononi serikali yetu katika kuninua sekta ya elimu hapa nchini. sote tunajua ya kwamba serikali yetu inaongozwa na sera ya serikali ya viwanda.


 Kwa maana hiyo hatuwezi kuwa na viwanda bila ya kuwa na wanasayansi, hiyo basi vitabu hivi vitaongeza chachu kwa wanafunzi wetu wa kuendelea kufanya vizuri katika masomo ya sayansi na hatimaye kufanikisha ndoto zao pamoja na serikali”.


Mh Kandege aliendelea kusema kwamba “nawaomba Airtel na wadau wengine waendelee kutusaidia kwenye nyaja zingine mbali mbali ili kuendelea kutengeneza mazingira bora kwa wanafunzi kujifunza na hivyo kuongeza uelewa na kuwa na taifa lenye ueledi”.


Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Airtel Rukwa na Katavi Bw, Hapson Kamanya  alisema “Airtel tunaamini jamii iliyoelimika inajengwa kutoka katika shule zenye vifaa vya kufundishia vya kutosha hususani vitabu,  ili kuwa na maendeleo endelevu ni muhimu kuwekeza kwenye elimu na leo tunathibitisha dhamira yetu kwa kutoa msaada wa vitabu katika shule hizi”.


Tunaamini ya kwamba msaada wa vitabu utachochea ufaulu mzuri katika masomo ya sayansi katika mkoa na  pia utaongeza idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi” Aliongeza Kamenya.


Kwa upande Mkuu wa shule ya Mwazye Bw, Haron Mwaibabu akiongea kwa niaba ya shule zilizofaidika na msaada wa vitabu hivyo alisema “Msaada huu umekuja wakati muafaka wakati shule zetu zimekuwa na upungufu wa vitabu na tunaahidi kuvitunza na kuvitumia ipasavyo".


Aliongeza, ni ukweli kuwa shule zetu zina uhaba wa vitabu vya sayansi kitu ambacho kilikuwa kinatupa ugumu kwenye kufundisha na hata kupelekea baadhi ya wanafunzi wetu kutotamani kuchukua masomo ya sayansi. Tunashukuru sana Airtel kwa kuwa mkombozi kwenye hili’.




No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages