.

ALIYEKUWA MGOMBEA UBUNGE KAWE AFARIKI DUNIA

Aug 24, 2017

DAR ES SALAAM
Aliyekuwa Mgombea Ubunge jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu uliopita, Colman Massawe (Pichani), amefariki Dunia.

Taarifa zilizopatikana zimesema, Massawe amefariki dunia jana asubuhi kutokana na ajali ya gari iliyomfika katika eneo la Bagamoyo mkoa wa Pwani.

Msiba upo Masaki ambako ndiko nyumbani kwa marehemu Massawe na mwili wake unatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช