Breaking News

Your Ad Spot

Aug 26, 2017

KINANA AMWANDALIA BALOZI WA CHINA HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI KUMUAGA

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimkabidhi zawadi maalum Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing, wakati wa hafla ya Chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga, Upanga jijini Dar es Salaam, leo Agosti 25, 2017. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, Naibu Spika Tulia Akson, Mabalozi kadhaa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, Mawaziri Kadhaa, Makatibu wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Makatibu wa Jumuia za Chama. Picha zote na Bashir Nkoromo.
 Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing akimshukuru Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana baada ya kupokea zawadi maluum, ambayo Kinana alimzawadia wakati wa chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza kabla ya kumkabidhi zawadi maalum Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing (kulia), wakati wa hafla ya Chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga, Upanga jijini Dar es Salaam, leo Agosti 27, 2017.
 Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing (kulia) akiifungua zawadi hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza wakati wa hafla hiyo.
  Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing (kulia) akizungumza wakati wa hafla hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing wakiinua glasi za vinwaji kabla ya kuzigonganisha kutakiana heri, wakati wa hafla ya Chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga, Upanga jijini Dar es Salaam, leo Agosti 27, 2017. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge Tulia Akson. Picha zote na Bashir Nkoromo.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akigonganisha glasi za viwanywaji na Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing kumtakia heri, wakati wa hafla ya Chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga, Upanga jijini Dar es Salaam, leo Agosti 27, 2017. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge Tulia Akson. Picha zote na Bashir Nkoromo.
  Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing akigonganisha glasi za vinywaji na Spika wa Bunge Tulia Akson kutakiana her,  wakati wa hafla ya Chakula cha jioni kilichoandaliwa na katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kumuaga Balozi huyo, Upanga jijini Dar es Salaam, leo Agosti 27, 2017. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu wa Bunge
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akigonganisha glasi za kinywaji na Waziri Jenista Mhagama wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Balozi Lu na wapili kulia ni Naibu Spika Tulia Akson.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akigonganisha Glasi na Balozi wa Zambia hapa nchini Judith Kangoma-Kapijimpanga wakati wa hafla hiyo.
Katibu wa Jumuia ya wanawake Tanzania Amina Makilagi, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Idara ya Uchumi na Fedha Dk. Frank Hawassi na kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka hamdu Shaka wakiwa na glasi za vinywaji vyao wakati wa hafla hiyo. KWA PICHA NYINGI ZA HAFLA HIYO/BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages