Breaking News

Your Ad Spot

Aug 13, 2017

MZEE MWINYI AWAASA WATUMIA VYOMBO VYA MOTO KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, akizungumza wakati wa Tamasha la Usalama Barabarani ambapo aliwaasa watumiaji wa vyombo vya moto kufuata heria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazosababisha ulemavu na vifo. Tamasha hilo limefanyika jana, Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, akisikiliza maelezo kutoka kwa Inspekta Ibrahim Samwix, wakati alipotembelea mabanda mbalimbali kwenye tamasha hilo.Kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni.
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, akisikiliza maelezo jinsi uvunjaji wa sheria za usalama barabarani unavyoweza kusababisha ajali, alipotembeleabanda la Maaskari wa usalama barabarani, kwenye hilo
Naibu Waziri Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,Mhandisi Hamad Masauni(kushoto), akimkabidhi tuzo Mgeni Rasmi,Rais Mstaafu wakati wa tamasha hilo
Kamishna wa Operesheni  naMafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Marijani(kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri Wizaraya Mambo ya  Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kwa kutambua mchango wake katika suala nzima la Usalama Barabarani. Kuliani Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi.PichanaWizaraya Mambo yaNdaniyaNchi
Balozi wa Usalama Barabarani, Samira Abuu(katikati), akiwa  katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi,Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi naNaibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, baada ya kupokea cheti cha kutambua mchango wake katika masuala ya Usalama Barabarani wakati waTamasha la Usalama Barabara nilililofanyika jana,Uwanjawa Uhuru, jijini Dar es Salaam.PichanaWizaraya Mambo yaNdaniyaNchi

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages