.

NAIBU WAZIRI WA ZAMANI MZEE DYAMWALE AFARIKI DUNIA

Aug 14, 2017

Mbunge Mstaafu wa Handeni na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii wa kipindi cha kwanza cha Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Mzee Hassan Chabanga Dyamwale (Pichani), amefariki dunia.

Mzee Dyamwale alikuwa mmoja wa Wataalam nguli wa mchezo wa soka na msomi wa falsafa ya mpira wa miguu.

Huyu ndiye mmoja wa Waasisi wa ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara. Katika ya miaka ya 80 Mzee Dyamwale chini ya Baraza la Michezo Tanzania pamoja na chama cha mpira wa miguu nchini enzi hizo FAT alianzisha programu maalum ya mpira kwa vijana na watoto mashuleni na mitaani iliyoitwa YOSSO.

Programu hii ilipata ufadhili wa serikali ya Norway ilisaidia sana vijana wengi kuvutika na mchezo wa soka.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช