.

RAIS DK. MAGUFULI NA RAIS MUSEVENI WAZINDUA MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA UGANDA HADI TANGA, LEO, MAKAONDA NA RUGE WAPATANISHWA.

Aug 5, 2017

 Rais Dk, John Magufuli na Rais Yoweri Museveni wa Uganda wakizindua Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Tanga, katika sherehe ya uzinduzi huo iliyofanyika leo katika eneo la Chongolani mkoani Tanga ambako mradi huo utajegwa. Kulia ni Makamu wa Rais samia Suluhu Hassan
  Rais Dk, John Magufuli na Rais Yoweri Museven wa Uganda wakikipongezana baada ya kuzindua Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Tanga, katika sherehe ya uzinduzi huo iliyofanyika leo katika eneo la Chongolani mkoani Tanga ambako mradi huo utajegwa. Kulia ni Makamu wa Rais samia Suluhu Hassan
 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akipeana mkono na Raais Yoweri Museveni wa Uganda wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Bomba hilo
 Wananchi wakishangiliaa wakati Rais Dk John Magufuli na Rais Yoweri Museni wa Uganda wakaizindua mradi huo
 Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye eneo la awali kabla ya kwenda meza kuu walipowasili kwenye sherehe za uzinduzi wa mradi huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Henry Shekifu na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
 aadhi ya wageni waalikwa
 Kikundi cha ngoma kikitumbuiza wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi huo
 Kikundi cha wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakitumbuiza wakati wa sherehe za auzinduzi wa mradi huo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana aakisalimia baada ya kukaribishwa na Makamu wa Raais Samia Suluhu Hassan (kushoto), jukwaani kama kiongozi Mkuu wa CCM. Wapili kushoto ni Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa.
 RAIS Dk. John Magufuli na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Kassim Majaliwa, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk.Medard Kalemani, akiwaeleza jambo wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi huo
 Rais Dk Magufuli akihutubia wakati wa uzinduzi wa mradi huo
Mkuu wa mkoa wa dar es Salaam Paul Makonda akaiapeana mkono na Mkurugenzi wa Clouds Media Ruge Mtahaba, wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi huo, baada ya Rais Dk. John Magufuli kuwaamuru kufanya hivyo jukwaani ili kuondoa uhasama uliopo baina yao,
 Rais Yoweri Museni akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mradi huo
 Rais Dk Magufuli na Rais Museveni wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii waliotumbuiza wakati wa sherehe hizo
 Rais Dk Magufuli na Rais Museven na viongozi wengine wakuu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii waliotumbuiza wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi huo
 Rais Dk Magufuli akiondoka na mgeni wake Rais Museveni baada ya kuzindua mradi huo
 Rais Dk Magufuli akiagana na mgeni wake Rais Museveni kabla ya mgeni huyo kuondoka kwenye uwanja wa Ndege wa mjini Tanga, baada ya sherehe za uzinduzi wa mradi huo
Rais Dk John Magufuli na mkewe Mama Janeti wakiungana na wengine kupunga mikono baada ya ndege iliyombeba Rais Yoweri Museni kuruka.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª