Breaking News

Your Ad Spot

Aug 12, 2017

RIDHIWANI ATOA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU ZA WILAYA YA BAGAMOYO

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akisalimiana na mchezaji anayeshiriki katika mashindano ya Kombe la Mazingira,yaliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na wabunge.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, akitoa vifaa kwa washiriki wa mashindano ya Kombe la Mazingira,yaliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na wabunge.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, akitoa vifaa kwa washiriki wa mashindano ya Kombe la Mazingira,yaliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na wabunge.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete wa tatu kutoka kulia akiwa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo wa pili toka kulia Majid Mwanga wakiangalia mashindano ya Kombe la Mazingira,yaliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na wabunge.

 Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akionyesha moja ya jezi  zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo l;a chalinze Ridhiwani Kikwete.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amegawa vifaa vya michezo kwa timu za jimbo hilo zinazoshiriki mashindano ya kombe la Mazingira linaloshirikisha timu za wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Ridhiwani, amesema kuwa atawapatia washindi wa pili wa michuano hiyo pikipiki ya miguu miwili na jezi kwa timu zote tatu za juu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga,ambaye pia ndio muaandaji wa mashindano hayo ametoa zawadi ya pikipiki ya Toyo ya miguu mitatu kwa mshindi wa kwanza ili itumike kwa shughuli za kuwaingizia kipato kwa vijana.


No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages