Breaking News

Your Ad Spot

Aug 21, 2017

UTAFITI WA KUGEMA UTOMVU WA KUTENGENEZEA BAZOKA (CHEWING GUM) NA GEL, SAO HILL

SAO HILL, TANZANIA
Shamba la miti la Sao Hill likishirikiana na Kampuni ya Art International limeanza utafiti wa kugema utomvu wa miti ya msindano kama njia ya kujiongezea kipato.



Akizungumza na Kamati ya Bunge ya Maliasili na Mabadiliko ya tabia ya nchi ya nchini Malawi iliyotembelea Shamba la Miti la Sao Hill,  Meneja wa Shamba hilo Salehe Beleko amesema katika kuongeza vyanzo vya mapato wameingia mkataba na kampuni hiyo kufanya utafiti na ikibainika kwamba haitaathiri ukuaji wala ubora wa miti wataidhinisha kuwa chanzo kipya cha mapato.



Akifafanua Salehe Baleko amesema wanatarajia kuuza kila kilo moja ya utomvu kwas h. 750.



Beleko amesema kwa kuwa ni utafiti wameanza kwanza na miti iliyokuwa tayari kuvunwa wakiona hakuna madhara wataendelea kwenye miti michache yenye umri mdogo na matokeo ya utafiti huo yatapelekea ama kukuza ama kukataza kabisa zoezi hilo.



Naye mtaalamu wa kampuni ya uchina, Yhoung Zhoung  amesema taasisi yake imefuata taratibu zote za ugemaji na usafirishaji wa utomvu huo na amefafanua kwamba kampuni yake inahitaji miti millioni mbili kwa mwaka ilikupata ujazo wa utomvu wanauhitaji



Akijibu swali la mke wa Rais wa zamani wa Malawi, Patricia Muluzi ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo ambaye alitaka kujua matumizi ya utomvu huo mtaalamu huyo amesema baada ya kuchakatwa na kuchanganywa na kemikali mbalimbali utomvu huo hutumika kutengenezea dawa mbalimbali bazoka (chewing gum) pamoja na gel





Mjumbe wa Kmaati hiyo, Rashid Pemba Msusa, amesema kwa mara ya kwanza wameshuhudia matumizi mapya kabisa ya zao la mti teknolojia ambayo hawajawahi kuiona nchini kwao Malawi. Hata hivyo ameahidi kufuatilia matokeo ya utafiti huo ili ukifaa wauhamishie Malawi
 Mtaalamu wa Kampuni ya Art International, Zhoung Yhoung akitoa maelezo kuhusu zoezi la ugemaji wa utomvu kwa ujumla unaofanywa na kampuni yake (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages