Breaking News

Your Ad Spot

Sep 11, 2017

RAIS DK. MAGUFULI AMUAPISHA JAJI MKUU FROF. IBRAHIM HAMIS JUMA, LEO

 Rais Dk. John Magufuli akimuapisha Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma  leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Profesa Ibrahim anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande na kuwa jaji wa nane kushika wadhifa huo tangu nchi ipate uhuru huku akiwa Mtanzania wa sita. Wapili kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa


Rais Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini hati ya kiapo cha Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahimu Hamisi Juma baada ya kumuapisha
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya kiapo Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahimu Hamisi Juma
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza baada ya kumuapisha Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Mhe. Profesa Ibrahimu Hamisi Juma leo
Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Profesa Ibrahimu Hamisi Juma akizungumza baada ya kuapishwa leo
 Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akizungumza baada ya Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Hamisi Juma kuapishwa

 Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi (kushoto) akiteta jambo na  Jaji Mkuu mstaafu Othman Chande (kulia) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju wakati wa hafla hiyo ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya majaji waliohudhuria hafla ya kumuapisha Jaji Mkuu wa Tanzania
 Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abbasi akifuatilia kwa makini hafla hiyo
 Jaji Kiongozi Ferdinand Wambali akiteta jambo na  Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande (kulia) wakati wa hafla hiyo
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa hafla hiyo. 

 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande baada ya kumuapisha Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Hamisi Jum. Kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumz na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi wakati wa hafla hiyo
 Rais Dk. John Magufuli akiwa na Jaji Mkuu na Spika wa Bunge wakati wa hafla hiyo

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma, Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai na Majaji mbalimbali, mwisho mwa hafla hiyo,leo Ikulu Jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages