.

DKT.FAUSTINE NDUGULILE AFUNGUA MKUTANO WA NNE WA CHAMA CHA WATAALAMU WA MAGONJWA YA FIGO MJINI DODOMA

Oct 30, 2017

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea kwenye mkutano wa wataalamu wa magonjwa ya figo nchini. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika kwenye Hotel ya Morena Mjini Dodoma na kuhudhuriwa na wataalamu mbalimbali kutoka Hospitali nchini, Wadau wa Maendeleo pamoja na wataalamu wengine kutoka nchi za Kenya, Sudan,India pamoja na Norway
Makamu wa Rais wa Chama cha wataalamu wa magonjwa ya Figo Tanzania (NESOT), Dkt. Paschal Ruggajjo akiongea dhima kubwa ya mkutano huo ni teknolojia ya upandikizaji wa viungo nchini ili kuweza kuhudumia wagonjwa takribani milioni 23.
Baadhi ya Wataalamu wa magonjwa ya figo waliohudhuria mkutano huo. Mkutano huo ni wa siku mbili ambapo watajadili dhana mbalimbali ya ugonjwa wa figo ikiwemo kutoa elimu kwa umma ili kuweza kukabiliana na magonjwa ya figo pamoja na upandikizaji.Tanzania imekua ikipeleka wastani wa wagonjwa thelathini na tano(35) kwa mwaka nje ya nchi kwa ajili ya kupandikiza figo na gharama ya kupandikiza nje ya nchi ikiwemo India ni shilingi milioni 75 hadi 77 kwa mtu mmoja ikiwemo kupandikiza, nauli pamoja na malazi
Makamu wa Rais wa Chama hicho Dkt. Paschal Ruggajjo (kulia) akimpa zawadi mmoja wa wataalamu wa figo ambaye amefanya tafiti na kuwasilisha mada ya katika mkutano huo Profesa Ainory Gesase ambaye ni mkufunzi wa Chuo cha Sayansi ya Tiba.
Picha ya pamoja ya Mgeni Rasmi wa mkutano huo Dkt. Ndugulile akiwa na wataalamu wa figo nchini pamoja na wadau wengine wa ndani ya nchi na nje ya nchi.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Ndugulile (aliye vaa koti la bluu) akisalimiana na washiriki katika Mkutano huo mara baada ya ufunguzi. alisema Serikali mgonjwa mmoja anahitaji wastani wa shilingi za kitanzania 37,620,504 kwa mwaka kwa ajili ya kulipia gharama za kusafisha damu nchini
Mashine za kusafisha figo(Dialysis Machine) ambazo zimefungwa kwenye hospitali nchini. Serikali imefunga mashine katika hospitali nchini ikiwemo UDOM (10),Hospitali ya Muhimbili (42), Hospitali ya Rufaa Mbeya(5), Hospitali ya Rufaa Bugando (10), KCMC(10),Hospitali ya Misheni Serian(10),Hospitali ya NSK Arusha(5),TMK(10),Regency(15),Hurbert Kairuki(5), Aga Khan(10) na Access(10).Mashine hizo zina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 783 kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) na 391 kwa huduma ya malipo ya papo kwa papo


Picha zote na Wizara ya Afya

WAZIRI MWAKYEMBE AZINDUA MAONYESHO YA MASHUJAA NA MAPAMBANO YA KUPATA UHURU

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ambayo yanalenga kuonyesha namna mashujaa wa Tanganyika walipambana kupata uhuru, maonyesho ambayo yatafanyika kwa muda wa mwezi mmoja katika Makumbusho ya Taifa- Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam. Uzinduzi wa maonyesho hayo ambao ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU), kwa lengo ya kuendeleza juhudi za Uhifadhi wa Hifadhi ya Urithi Tanzania,hususani ya Ukombozi wa Afrika yanasimamiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa maonyesho hayo, Dkt. Mwakyembe alisema mradi huo wa kuhifadhi historia ya Ukombozi wa bara la Afrika ni muhimu kwa Tanzania kwani unaweza kusaidia kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea nchini kuliko ilivyo sasa kwani inawapa nafasi wageni ya kuona mambo tofauti na yaliyozoeleka pindi wanapokuja nchini. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ya kupata Uhuru. “Tuna mradi ambao utatupeleka mbali sana Watanzania, Afrika Kusini, Namibia, Angola hata wao wametuambia tusije shangaa sehemu hiyo ikawa inaleta watalii wengi zaidi kuliko wanaokuja kuangalia tembo na simba, urithi wa Afrika tumekabidhiwa na bara la Afrika ni wajibu wetu Watanzania kuusukuma huu mradi maana tumeshachelewa, Watanzania wengi labda hawaelewi mwaka 2011 kwa kushirikiana na UNESCO tulipeleka ombi AU la mradi huu wa bara la Afrika na wakaubariki huu mradi na wakaamua makao makuu yawe Tanzania na sisi tukachagua Dar na hapa kitajengwa kituo kikubwa kitakuwa na historia ya Ukombozi wa Afrika, sisi ndiyo viongozi wa huu mradi,” alisema Dkt. Mwakyembe. Alisema ili kufanikisha mradi huo tayari wameanza kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha pindi watakapojenga kituoambacho kitatumika kuhifadhi vitu mbalimbali ambavyo vilitumika katika kipindi cha ukombozi wa bara la Afrika kuwe na taarifa nyingi kuhusu bara la Afrika. “Tunawatumia wazee walio na historia ya ukombozi wa Afrika tumehoji zaidi ya wazee 100 na tunaendelea na hilo zoezi na tumebaini maeneo zaidi ya 200 Tanzania ambayo yanahitaji kuhifadhiwa, ni wajibu wangu kupeleka muswada bungeni ili tuyahifadhi na kuyalinda kwa kutumia sheria,” alisema Waziri Mwakyembe. Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya nchini (EU), Roeland Van de Geer akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ya kupata Uhuru. Kwa upande wa Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya nchini (EU), Roeland Van de Geer alisema ni muhimu kwa bara la Afrika kuwa na maonyesho ambayo yanaelezea historia ya bara hilo ili yatumike kuelezea kizazi cha sasa na kijacho namna nchi za Afrika zilipambana kupata uhuru na wao kama EU wataendelea kusaidia miradi mbalimbali yenye lengo ya kutunza urithi wa bara la Afrika. “Ni jambo la kujivunia kwa Umoja wa nchi za Ulaya kusaidia kufanikisha mradi huu … EU tumekuwa tukisaidia miradi mingi na hii yote ni kwa ajili ya kutunza utamaduni na urithi wa bara la Afrika, tumesaidia miradi mbalimbali nchini ikiwepo ya Olduvai na Ngorongoro na tutaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuendeleza maeneo ya kihistoria,” alisema. Afisa Mpango Kitaifa wa UNESCO, Nancy Kaizilege akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ya kupata Uhuru. Naye Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki na Afisa Mwakilishi wa Unesco Dar, Ann Therese Ndong- Jatta katika hotuba yake iliyosomwa na Afisa Mpango Kitaifa wa UNESCO, Nancy Kaizilege alisema ni jambo zuri kuwepo na makumbusho ambayo yanaeleza historia ya bara la Afrika na yatawza kuwapa nafasi watu mbalimbali kutoka mataifa ya nje ya bara la Afrika kuona na kujifunza historia ya Afrika. “Makumbusho haya ni muhimu kwasababu ni sehemu ya ukumbusho wetu kwa baadae, kupitia makumbusho haya tutaona historia ya bara la Afrika, historia ya mwanadamu na safari ya kutafuta uhuru ilivyokuwa,” alisema Kaizilege. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya nchini (EU), Roeland Van de Geer wakikata utepe katika uzinduzi wa Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ya kupata Uhuru.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa ameongozana na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya nchini (EU), Roeland Van de Geer na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kuangalia vitu mbalimbali vya kihistoria ambavyo vimewekwa katikaMaonyesho ya Mashujaa na Mapambano ya kupata Uhuru.SERIKIALI: TAARIFA ZA TAKWIMU ZA PATO LA TAIFA ZA ZITTO NI ZA UWONGO

Mkurugenzi wa Sera na Tafiti toka Benki Kuu Johnson Nyella (kushoto)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo ichani) wakati akikanusha taarifa za upotoshaji kuhusu takwimu za pato lataifa mapema hii leo jijini Dar es Salaam
<<<
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Serikali imetoa onyo kali kwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe juu ya taarifa za upotoshaji wa takwimu za pato la taifa alizozitoa hivi karibuni.

Taarifa hizo za  Zitto zimeripoti kuwa ukuaji wa pato la taifa kwa robo ya pili ya mwaka 2017 kuwa ni asilimia 5.7 badala ya asilimia 7.8. Kasi ya ukuaji ya asilimia 5.7 ilikuwa ni kwa robo ya kwanza ya Januari hadi Machi 2017.

Onyo hilo limetolewa leo Jijini Dar es Salaam na  Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa kutoka Ofisi ya Taifa za Takwimu (NBS) Daniel Masolwa, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NBS, pamoja na  Mkurugenzi wa Sera na Tafiti za Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania, Johnson Nyella wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari.

Masolwa amesema kuwa upotoshaji huo uliofanywa na  Zitto ni wa makusudi na unalenga kuonesha kuwa juhudi znazofanywa na Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli, hazina manufaa kwa Wananchi.

“Napenda kukanusha kauli ya Zitto kuhusu taarifa zake zinazodai kuwa takwimu za pato la taifa zimepikwa, Zitto anatakiwa kujua kwamba kazi ya kukokotoa takwimu za Pato la Taifa ni ya kitaalam na inafuata miongozo inayotolewa na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Takwimu na Shirika la Fedha Duniani (IMF)”,alisema Masolwa.

Ameongeza kuwa miongozo hiyo ni pamoja na mifumo ya pato la Taifa ya mwaka 2003 na 2008 na mwongozo wa kuainisha shughuli za kiuchumi Toleo la Nne ambapo kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia ya mwaka  2016 Tanzania imekuwa nchi ya pili kwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara kwa utoaji, uchambuzi, usimamizi na usambazaji wa takwimu  kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Aidha Bw.Masolwa ametoa wito kwa taasisi yoyote ile au mtu binafsi anayetaka kutayarisha takwimu rasmi  kwa ajili ya kutunga sera na kupanga mipango ya maendeleo kupata maelezo ya kina kuhusu ukokotoaji na miongozo mbalimbali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sera na Tafiti za Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania, Johnson Nyella amesema kuwa Mh. Zitto amekokotoa ukuaji wa Pato la Taifa anaodai kuwa ni sahihi kwa kuangalia tofauti kati ya ongezeko la ujazi wa fedha na mfumuko wa bei jambo ambalo sio sahihi kulitumia kama kipimo.

“Ukokotoaji wa aina hiyo umejengwa juu ya nadharia inayoitwa ‘quantity theory of money’ ambayo inasema mfumuko wa bei hutokea pale fedha zinapoongezeka kwa kasi zaidi kuliko uzalishaji wa vitu halisi ambayo si sahihi kutumia nadharia hiyo kuelezea mfumuko wa bei na ukuaji wa uchumi katika kipindi cha muda mfupi kama Mh. Zitto alivyofanya,” alifafanua Bw.Nyella.

Wawakilishi hao wa Benki Kuu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wamelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya taarifa za Ukuaji wa Pato la taifa kutolewa na Mh.Zito, na wakawaasa Wananchi na wanasiasa kuacha kupotosha takwimu za serikali na kuziomba mamlaka husika kuchukua hatua kwa yeyote atakayebainika kupotosha umma kwa makusudi.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA SERA YA TAIFA YA HUDUMA NDOGO YA FEDHA MJINI DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akionyesha kitabu cha sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2017 pamoja na Mkakati wa Utekelezaji mara baada ya kukizindua kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip  Mpango na Mkurugenzi Mtendaji wa FSDT Bw. Sosthenes Kewe.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2017 pamoja na Mkakati wa Utekelezaji uliofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

RAIS DK. MAGUFULI AFUNGUA DARAJA LA WAENDA KWA MIGUU LA FURAHISHA JIJINI MWANZA

 Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella pamoja na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha liliopo jijini Mwanza
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na viongozi mbalimbali akivuta utepe kwenye jiwe la ufunguzi kuashiria ufunguzi wa wa Daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha liliopo jijini Mwanza
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kufungua daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha jijini Mwanza
 Sehemu ya umati wa wananchi waliohudhuria ufunguzi wa daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha jijini Mwanza.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi kabla ya ufunguzi wa daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha jijini Mwanza 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma na kikundi cha ngoma za asili cha jijini Mwanza mara baada ya ufunguzi wa daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha jijini Mwanza
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia pamoja na wananchi waliohudhuria katika sherehe za ufunguzi wa wa daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha jijini Mwanza.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wakati akiwaaga mara baada ya ufunguzi wa Daraja hilo la Furahisha
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kabla ya ufunguzi wa daraja hilo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwaaga wananchi katika eneo la Daraja la Furahisha jijini Mwanza mara baada ya ufunguzi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza

LAZARO NYALANDU ASHINDWA KASI YA RAIS MAGUFULI, AACHIA NGAZI UBUNGE, LEO


RAIS DK MAGUFULI AENDA MWANZA LEO

Rais Dk. John Magufuli akiagana na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kabla ya kuondoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kwenda mkoani Mwanza leo.


DAR ES SALAAM
Rais Dk. John Magufuli, leo Jumatatu, Oktoba 30, 2017, ameondoka jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Mwanza, ambapo akiwa mkoani humo pamoja na mambo mengine atafungua mradi wa ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu lililopo eneo la Furahisha.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu, imesema pia Rais Magufuli atafungua kiwanda cha iinywaji baridi cha Sayona kilichopo Nyakato mkoani humo na baadaye kufanya mkutano wa hadhara.

Katika Uwanja wa Ndege wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Rais Magufuli ameagwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

AMUUA MTOTO WAKE KWA RISASI AKIPAMBANA NA POLISI

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
Mkazi mmoja wa Lukenge katika mkoa wa Pwani, Ally Sakalawe (43) amemuua mtoto wake na kumjeruhi Polisi baada ya kupiga risasi hivyo akikaidi kujisalimisha kwa makachero wa polisi waliokwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Blasilus Chatanda amethibitisha kutokea tukio hilo na kufafanua kuwa mtoto aliyeuawa ametambuliwa kuwa ni Mekwere Ally na akari polisi aliyejeruhiwa ni F 3438 D/CPL Leonard ambaye risasi ilimpata mkono wa kushoto.

Alifafanua, Kaimu kamanda alisema siku hiyo mkuu wa upelelezi Mkoa wa Pwani SSP Kingai akiwa na timu ya makachero walimkamata Sakalawe, akiwa na bunduki mbili aina ya gobore, risasi mark 4 na kipande kimoja cha gamba la kakakuona.

Alitaja vitu vingine kuwa ni vipande kumi vya nondo vilivyokatwa mithili ya risasi, goroli 249 za baiskeli alizokuwa anatumia kama risasi na vifurushi saba vya nyuzi ya katani alizokuwa akitumia kwenye mtutu wa bunduki kuzuia baruti.

Chatanda alielezea, katika upekuzi askari walijitambulisha kwa watu waliokuwa ndani ya nyumba hiyo kwa kuwataka wajisalimishe lakini Ally Sakalawe alikaidi na kuamua kufyatua risasi ovyo .

"Kati ya risasi hizo alizokuwa akifyatua alimjeruhi tumboni mtoto wake anaeitwa Mekwere Ally ambae alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu kituo cha afya Chalinze, na pia alimjeruhi askari F 3438 D/CPL Leonard katika mkono wake wa kushoto na  amepatiwa matibabu katika kituo cha afya Chalinze na amesharuhusiwa " alisema Chatanda. 

MAGAZETI YA NDANI NA NJE YA TANZANIA LEO OKTOBA 30,2017


Magazeti zaidi>Bofya Hapa

CCM YAZINDUA KWA KISHINDO KAMPENI ZA UDIWANI KIJICHI LEO, KUSILAWE ASEMA CCM ITASHINDA UDIWANI KATA ZOTE TATU DAR

Oct 29, 2017

 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe akimnadi mgombea wa CCM katika uchaguzi wa marudio wa Udiwani Kata ya Kijichi, Eliasa Mtalawanje,Temeke Dar es Salaam, leo. Akizungumza amesema CCM itashinda Udiwani kata zote tatu ambako uchaguzi unarudiwa mkoani Dar es Salaam. Kata zingine ni Saranga na Mbweni.
 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe akiwasili kwenye Uwanja wa mkutano kuzindua kampeni za Uchaguzi mdogo wa Udiwani kata ya Kijichi, leo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke Almishi Hazal
 Wananchi na wana CCM wakishangilia wakati Kusilawe na viongozi wenzake wakiingia Uwanjani
 Vijana wa hamasa wakichangamsha mkutano huo
 Madansa wakicheza muziki kuchangamsha mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni za CCM za Udiwani kata ya Kijichi.
 Mgombea Udiwani kwa tiketi ya CCM kata ya Kijichi Eliasa Mtalawanje akisalimia baada ya kutambulishwa kutambulishwa kwenye mkutano huo
 Mtalawanje akitroti baada ya kutambulishwa na Mwenyekiti wa Wazee wa CCM Temeke
 Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM Wilaya ya Temeke Mohammed Mbonde, akizungumza baada ya kukaribishwa jukwaani kusalimia.
 Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Wilaya ya Temeke Mohammed Mbonde, akipongezwa na Mgombea Udiwani kata ya Kijichi Eliasa Mtalawanje baada ya kutoka jukwaani kusalimia.
 Meya wa Temeke Abdallah Chaurembo akisalimia wananchi kwenye mkutano huo, na kuzungumza kuhusu umuhimu wa wananchi kumchagua mgombea wa CCM Udiwani kata ya Kijichi.
 Mbunge wa Mbagala Issa Mangungu, akisalimia wananchi kwenye mkutano huo, na kuzungumza kuhusu umuhimu wa wananchi kumchagua mgombea wa CCM Udiwani kata ya Kijichi.
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke Almishi Hazal akisalimia wananchi na kumkaribisha Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, kuhutubia mkutano huo na kumtambulisha mgombea wa CCM wa Udiwani Kata ya Kijichi
 Vijana wa hamasa na wananchi wakiwa wametulia kumsikiliza 
 Baadhi ya wananchi kwenye mkutano huo
 Viongozi wa Barza la wazee Temeke wakiwa kwenye mkutano huo
 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Saad Kusilawe akihutubia mkutano huo
 Kusilawe akisisitiza jambo
 Vijana wa CCM wakimshangilia Kusilawe
 Msimamizi wa uchaguzi wa CCM makao makuu Mzee Kazidi (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Wilaya ya Temeke Almishi Hazal. katikati ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam
 Mzee Kazidi akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Kuslawe.
 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe akimnadi mgombea wa CCM katika uchaguzi wa marudio wa Udiwani Kata ya Kijichi, Eliasa Mtalawanje,Temeke Dar es Salaam, leo  
 Kisha akamkabidhi mgombea huyo ilani ya CCM
 Kusilawe akimkabidhi ilani mgombea huyo
 Mgombea akionyesha ilani baada ya kukabidhiwa
 Mgombea wa CCM katika uchaguzi wa marudio wa Udiwani Kata ya Kijichi, Eliasa Mtalawanje,Temeke Dar es Salaam, akizungumza na kuomba kura baada ya kunadiwa na Kusilawe, leo
 Eliasa Mtalawanje akifafanua jambo kwa makini
 Wananchi wakimshangilia mgombea huyo
 Mgombea huyo akiendelea kuomba kura kwa wananchi 
Mgombea wa CCM katika uchaguzi wa marudio wa Udiwani Kata ya Kijichi, Eliasa Mtalawanje,Temeke Dar es Salaam, akiondoka uwanjani mwishoni mwa mkutano. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
ยช