.

MAGAZETI YOTE YA LEO JUMATATU, JANUARI 29, 2018

Jan 29, 2018

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, DKT. JUMA MALEWA ATETA NA MAHABUSU GEREZA LA KEKO: NI SEHEMU YA WIKI YA SHERIA NCHINI

 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akimsikiliza Mahabusu ambaye ni raia wa kigeni alipotembelea  gereza la Keko jijini Dar es Salaam leo Januari 28, 2018.

.
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akisalimiana na Mkuu wa Gereza la Mahabusu Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kiangi Abdallah alipowasili katika ziara yake ya kikazi kukagua gereza hilo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria hapa nchini. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo.
 Mkuu wa Gereza la Mahabusu Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kiangi Abdallah akitoa taarifa fupi mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa kabla ya kumkaribisha kuongea na Mahabusu wa Gereza Keko(hawapo pichani).
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiongea na Mahabusu wa Gereza Keko(awapo pichani) leo Januari 28, 2018 alipotembelea gereza hilo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria hapa nchini.
 Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiwa katika chumba Maalum, Gereza Keko ambapo chumba hicho kitatumika katika Uendeshaji wa Mashauli mbalimbali kwa kutumia njia ya TEHAMA. Uwepo wa mfumo huu utalipunguzia gharama Jeshi la Magereza katika kuwasafirisha Mahabusu mahakamani na kuwarejesha magerezani.
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika Chumba Maalum ambacho kitatumika katika uendeshaji wa mashauli kwa kutumia njia ya  TEHAMA(wa kwanza kushoto) ni  Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Noel James(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Gereza Keko, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kiangi Abdallah 
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiwasili katika Gereza la Mahabusu Keko jijini Dar es salaam katika ziara yake ya kikazi kukagua gereza hilo leo Januari 28, 2018 ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria hapa nchini. Jeshi la Magereza ni moja ya wadau muhimu katika sekta ya Sheria hapa nchini.(PICHA ZOTE NA JESHI LA MAGEREZA).

RAIS MAGUFULI NA MAMA JANETH MAGUFULI WATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MWILI WA MAREHEMU JAJI MSTAAFU ROBERT KISANGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Januari 28, 2018 ametia saini kitabu cha maombolezo na kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwake Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pia wametoa mkono wa pole kwa mke wa Marehemu Mama Maria Kisanga na kufanya maombi ya pamoja na familia ya marehemu.
Jaji Mstaafu Robert Kisanga alifariki dunia tarehe 23 Januari, 2018 katika hospitali ya Regency Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimfariji mjane wa marehemu Mama Maria Kisanga baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa  Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam,  Januari 28, 208.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na mtoto wa marehemu, Amani Kisanga, baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam, Januari 28, 2018. kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma na kulia ni Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakifanya maombi pamoja na mjane wa marehemu Mama Maria Kisanga na mtoto wa marehemu Amani Kisanga na waombolezaji wengine baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam . 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam. 
 Mama Janeth Magufuli akimfariji mjane wa marehemu Mama Maria Kisanga baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo na kisha kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam
 Waheshimiwa Majaji na waombolezaji wengine wakiwa kwenye msiba wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Mstaafu Joseph sinde Warioba  baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwa marehemu  Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA IKULU)
ยช