.

BARAZA LA MABALOZI WA KIARABU – TANZANIA

Jan 12, 2018

Baraza la Mabalozi wa Kiarabu nchini Tanzania linathamini upigaji kura wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha rasimu ya azimio linalohusu Mji wa Jerusalem, lililopitishwa  Alhamisi  ya tarehe 21 Desemba 2017, katika utaratibu wa  Kikao cha Kumi  Maalumu cha Dharura cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, chini ya kichwa cha habari kisemacho “Matendo ya Israeli yasiyo ya kisheria Jerusalem ya Mashariki inayokaliwa kimabavu na maeneo mengine ya Palestina yanayokaliwa kimabavu”, azimio lililopitishwa baada ya nchi 128 kulipigia kura ya ndio, huku nchi 9 zikilipinga ikiwemo Marekani na Israeli.
Kwa mnasaba huu, Baraza na Mabalozi wa Kiarabu linatilia mkazo kuthamini kwake msimamo huu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, nao ni msimamo unaoonesha hali ya kwenda sambamba na misingi muhimu iliyowekwa na Kiongozi Muasisi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, katika yale yahusuyo kuheshimu uhalali wa kimataifa na haki za mataifa katika kujipangia mustakabali wake na kukabiliana na ukoloni na uvamizi wa kigeni.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª