Breaking News

Your Ad Spot

Jan 24, 2018

RAIS DK MAGUFULI AMLILIA JAJI MSTAAFU ROBERT KISANGA

IKULU DAR ES SALAAM
Rais Dk John magufuli amemtumi asalamu  za rambirambi JajiMkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma kufuatia kifo cha Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Robert Kisanga kilichotokea jana Januari 23, 2018 katika hospitali ya Regency Jijini Dar es Salaam.

Katika salamu hizo Rais Magufuli (Pichani), amesema Jaji Mstaafu Robert Kisanga atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa kwaTaifa wakati wote wa utumishi wake uliojaa umakini, uchapakazi, uzalendo na ushirikiano na wengine, mambo ambayoyalimwezesha kupata mafanikio makubwa.

“Sote tunafahamu kazi nzuri alizofanya akiwa katika majukumu mbalimbali ya kitaifa, mchango wake katika uijenga taaluma ya uanasheria baada ya uhuru na uanzishajiwa Mahakama ya Rufani baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977, kwa hakika mchango wake hautasahaulika.

“Nakuomba Mhe. Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma unifikishie salamu zangu za pole kwa familia ya Marehemu Jaji Mstaafu Kisanga, Majaji na wanasheria wote, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu” amesema  Rais Magufuli.

Rais Magufuli amewaombea wafiwa wote wawe na moyo wasubira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na amemuombea Marehemu Jaji Mstaafu Kisanga apumzishwe mahali pema peponi.

Marehemu jaji Mstaafu Robert Kisanga

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages