Breaking News

Your Ad Spot

Feb 10, 2018

RAIS DK. MAGUFULI AMPANDISHA CHEO ALIYEKUWA MHASIBU MKUU WA POLISI ZANZIBAR NA KUMTEUA KUWA KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR

Ikulu,  Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Februari, 2018 amempandisha cheo na kumteua aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Polisi Zanzibar Bw. Mohamed Hassan Haji kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imefafanua kuwa Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo Bw. Mohamed Hassan Haji kutoka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna wa Polisi (CP), na kisha kumteua kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.

Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji amepandishwa cheo na kuteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar kuanzia leo tarehe 10 Februari, 2018.

Kabla ya uteuzi huu Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji alikuwa Mhasibu Mkuu wa Polisi Zanzibar.

Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Hamad Omar Makame ambaye amestaafu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages