.

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ASHIRIKI MKUTANO WA TOKOMEZA MALARIA

Sep 28, 2018

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya  Kikwete ameshiriki katika mkutano wa Baraza la Kutokomeza Malaria Duniani (End Malaria Council) uliofanyika tarehe 26 Septemba, 2018 mjini New York Marekani.

Baraza la Kutokomeza Malaria linaundwa na Wajumbe 9 ambao ni watu mashuhuri katika sekta ya umma na sekta binafsi chini uenyekiti wa Bill Gates. 


Lengo la Baraza hilo ni kuunganisha nguvu za wadau na mataifa duniani kukabiliana na hatimaye kutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2030.

ZOEZI LA KUSAJILI WAKAAZI WA ZANZIBAR KATIKA MFUMO WA KIELEKTRONI (E-ID CARD) LAANZA

Sep 9, 2018

 Zoezi la uandikishaji wananchi wa Zanzibari katika mfumo wa kidigitali limeanza rasmi  Sept 8, 2018 katika Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja. Ambapo idadi kubwa ya wananchi imejitokeza kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho ya kielektroniki (E-ID CARD). 

Mapema wiki hii rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein alizindua Vituo vya Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibar na Uzinduzi wa Uimarishaji Mfumo wa Usajili kielektroniki hafla iliofanyika katika viwanja vya Ofisi hiyo Dunga Wilaya ya Kati Unguja.

Ambapo lengo la mfumo huo ni kuifadhi taarifa katika mfumo wa kisasa ili kurahisisha hupatikanaji huduma na taarifa pindi zinapohitajika. Zoezi hilo limeanza katika vituo tofauti vya Skuli ya Dunga Kiembeni,kituo cha Dunga Bweni katika skuli ya Maandalizi na kituo cha Skuli ya Mpapa vyote katika Mkoa wa Kusini.
Wananchi wakiendelea kuandikishwa.
Mwitikio wa wananchi ulikuwa ni mkubwa sana.
ยช