.

MTANDAO WA ELIMU WA TESEApp WAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

Oct 10, 2018



Muanzilishi wa TESEApp Abdul Mombokaleo, akionyesha Tablet ambayo mwanafunzi anaweza kutumia katika kusoma katika mtandao wa TESEA  ikiwa tayari imewekwa mtandao maalumu wa masomo ya sekondari (Kidato 1 - 4) na (kidato 5 - 6) akiwa na  Mwenyekiti wa Taifa wa wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini (TAMONGSCO) Ndugu Charles Totera katika uzinduzi wa TESEApp.


Muanzilishi wa TESEApp Abdul Mombokaleo, akionyesha Tablet ambayo mwanafunzi anaweza kutumia katika kusoma katika mtandao wa TESEA  ikiwa tayari imewekwa mtandao maalumu wa masomo ya sekondari (Kidato 1 - 4) na (kidato 5 - 6) akiwa na  Mwenyekiti wa Taifa wa wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini (TAMONGSCO) Ndugu Charles Totera katika uzinduzi wa TESEApp.
Muanzilishi wa TESEApp Abdul Mombokaleo wa kulia akisalimiana na Mwenyekiti wa Taifa wa wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini (TAMONGSCO) Ndugu Charles Totera katika uzinduzi wa TESEApp.  





Muanzilishi wa TESEApp Abdul Mombokaleo akizungumza katika uzinduzi wa TESEApp.


Baadhi ya wadau elimu na Walimu wa shule mbalimbali jijini Dar es Salaam wakifatilia kwa makini uzinduzi wa mtandao wa elimu wa TESEApp.


Muanzilishi wa mtandao wa Elimu wa Tesea Abdul Mombokaleo amesema kuwa msingi wa kuanzishwa kwa mtandao wa Tesea ni kurahisisha upatikanaji wa marejeo(notes) kwa wanafunzi kujifunza na kupata elimu kwa kutumia teknolojia ya kisasa.


Amesema mtandao huu utakuwa na marejeo(notes) zote za kutosha  na ambayo yame hakikiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania ili kusaidia wanafunzi kupata marejeo yanayotakiwa katika masomo yao.


"mtandao huu hauchukui nafasi ya mwalimu bali utamsaidia mwalimu kuandaa masomo kwa urahisi kwani notes hizo zinafata mtaala wa serikali kwa kuwa na silabasi zote zinazotakiwa kwa mwanafunzi kujifunza awapo shuleni". amesema Mombokaleo


Amesema mtandao huo unaopatika kupitia simu za smartphone,laptop,tablet na computer za mezani na unaweza kupakuliwa kiurahisi na mwanafunzi kijisali na kuanza kutumia mtandao kwa gharama nafuu,na kupata masomo yote ya biashara,sayansi na elimu za dini ya kiislamu na kikristo pamoja na mitihani iliyopita (pastpapers).  


Kwa upande Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa taifa wa wamiliki wa shule binafsi nchini Charles Totera, amesema kuwa elimu inatakiwa kumsaidia mtu kuweza kutatua matatizo yake bila kusubiri msaada kutoka kwa mtu mwingine  kwa uwezo wake wa kufikiri kutokana na elimu aliyonayo.


Amesema kuwa Wizara ya Elimu iache kuwazawadia watu wano karirishwa katika elimu na badala yake kuwapa motisha watu wanakuja na ubunifu ambao unakuwa msaada kwa wengine kwani anafurahi kuona vijana wanatumia tekinolojia kufanya mambo ambayo ni msaada kwa Taifa.


"Elimu ya kukaririsha wanafunzi inaua vipaji na kudumaza akili za wale ambao wanachukia kukariri napiga vita elimu ya kukariri haisadii mtu,nchi wala hata msomi mwenyewe"amesema Totera


Amesema kuwa mtandao huo utasaidia wanafunzi hasa wale ambao wanasoma wenyewe bila mwalimu na ambao hawana vifaa vya kujisomea kupitia mtando huo watapata elimu kamilifu na timilifu na kuwaasa walimu kuacha tabia za kukaririsha wanafunzi kwa ajili ya kufaulu mitihani.




NAMNA YA KUPAKUA NA KUJIUNGA TESEApp
1.Pakua TESEApp kutoka Google play (kupitia Android Devices)
au App Store (kwa iOS Devices)
2. Jiandikishe au jisajili kwa ajili ya kuingia (Sign Up)
3. Chagua Kifurushi Unachohitaji






4. Jifunze na Ufurahie





RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ASHIRIKI MKUTANO WA TOKOMEZA MALARIA

Sep 28, 2018

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya  Kikwete ameshiriki katika mkutano wa Baraza la Kutokomeza Malaria Duniani (End Malaria Council) uliofanyika tarehe 26 Septemba, 2018 mjini New York Marekani.

Baraza la Kutokomeza Malaria linaundwa na Wajumbe 9 ambao ni watu mashuhuri katika sekta ya umma na sekta binafsi chini uenyekiti wa Bill Gates. 


Lengo la Baraza hilo ni kuunganisha nguvu za wadau na mataifa duniani kukabiliana na hatimaye kutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2030.

ZOEZI LA KUSAJILI WAKAAZI WA ZANZIBAR KATIKA MFUMO WA KIELEKTRONI (E-ID CARD) LAANZA

Sep 9, 2018

 Zoezi la uandikishaji wananchi wa Zanzibari katika mfumo wa kidigitali limeanza rasmi  Sept 8, 2018 katika Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja. Ambapo idadi kubwa ya wananchi imejitokeza kujiandikisha ili waweze kupata kitambulisho ya kielektroniki (E-ID CARD). 

Mapema wiki hii rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein alizindua Vituo vya Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibar na Uzinduzi wa Uimarishaji Mfumo wa Usajili kielektroniki hafla iliofanyika katika viwanja vya Ofisi hiyo Dunga Wilaya ya Kati Unguja.

Ambapo lengo la mfumo huo ni kuifadhi taarifa katika mfumo wa kisasa ili kurahisisha hupatikanaji huduma na taarifa pindi zinapohitajika. Zoezi hilo limeanza katika vituo tofauti vya Skuli ya Dunga Kiembeni,kituo cha Dunga Bweni katika skuli ya Maandalizi na kituo cha Skuli ya Mpapa vyote katika Mkoa wa Kusini.
Wananchi wakiendelea kuandikishwa.
Mwitikio wa wananchi ulikuwa ni mkubwa sana.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI SUBIRA MGALU, ATEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MITA ZA LUKU ZA KISASA JIJINI DAR ES SALAAM

Jun 8, 2018


 NAIBU Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, akiwa ameshika moja ya mita ya kisasa ya LUKU, (Smart Meter), iliyotengenezwa na kiwanda cha Baobab Engineering System Tanzania kilichoko Mbezi jijini Dar es Salaam, wakati alipokitembelea kujionea mita hizo leo Juni 8, 2018.
  NA K-VIS BLOG/KhalfanSaid

NAIBU Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, ametembelea kiwanda cha kutengeneza mita za LUKU kilichoko Mbezi jijini Dar es Salaam leo Juni 8, 2018 na kuridhishwa na ubora wa mita hizo.

Alisema tatizo la mita lilikuwa ni changamoto kubwa iliyopelekea kasi ya kuwafikishia umeme Watanzania kuwa na kikwazo kwani TANESCO iliagiza mita hizo kutoka nje.

Kampuni ya Baobab Engineering System Tanzania ndiyo watengenezaji wa mita hizo za kisasa za  LUKU (Smart Meters) na uongozi wa kiwanda umeahidi kuzalisha mita za kutosha ili kutatua changamoto iliyokuwa ikiikabili TANESCO kuhusu upatikanaji wa mita.

“Sisi katika kutaka shirika letu la TANESCO lifanye vizuri tumewapa maelekezo yako ndani ya Sera na mipango yetu lazima waunganishie umeme wateja wengi na moja ya component inayotakiwa ni mita, kumekuwa na changamoto ya mita kama mlivyosema, na hasa inatokana na utaratibu wa uagizaji na hata kufika kwa vifaa hivyo ilichukua muda sana, sasa uwepo wa kiwanda cha kutengeneza mita hapa nyumbani ninaamini tatizo hili sasa halitakuwepo.” Alisema Mhe. Naibu Waziri Mgalu.

Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshuhghulikia Mauzo na Masoko Mhandisi Theodory Bayona amesema, tayari Shirika limeanza kutekeleza agizo hilo la serikali na mchakato wa manunuzi umeanza kwa kuhakikisha vifaa vyote vya Shirika vinanunuliwa kutoka ndani na tayari TANESCO imeanza kwa kununua nguzo za umeme hapa hapa nchini, lakini kuhusu mita za umeme TANESCO inampango wa kununua mita 350,000 kutoka kwa wawekezaji wa ndani na mita hizo hasa zitatumika kubadilisha zile mita zile za zamani ambapo zilikuwa haziendi sawasawa lakinin pia kuwaunga na wateja wapya., Alisema Mhandisi Bayona.

Awali Mhe. Naibu Waziri alipatiwa maelezo ya kiuntendaji ya kiwanda hicho kabla ya kupata fursa ya kutembelea eneo la uzalishaji na kujionea jinsi mafundi wazawa wa kiwanda hicho wanavyotengeneza mita hizo la LUKU

 Mheshimiwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizunguzma jambo baada ya kujionea mita hizo.
 Mhe. Naibu Waziri akimsikiliza Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshuhghulikia Mauzo na Masoko, Mhandisi Theodory Bayona.
 Wataalamu wa kiwanda ambao wote ni Watanzania wakiwa kazini.
 Mhe. Naibu Waziri akiangalia utaalamu wa kutengeneza mitab hizo.
 Mhe. Naibu Waziri akiangalia utaalamu wa kutengeneza mitab hizo.
 Moja ya mita hizo ikiwa katika hatua za mwisho za matengenezo.
 Wataalamu wa kiwanda ambao wote ni Watanzania wakiwa kazini.
 Wataalamu wa kiwanda ambao wote ni Watanzania wakiwa kazini.
 Mhe. Subira Mgalu, akizunhuzma. Kulia ni Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshuhhulikia Mauzo na Masoko, Mhandisi Theodory Bayona.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwanda cha Baobab Engineering System Tanzania, Bw.Allan Magoma, akizungumza.
Picha ya pamoja 

DK MNDOLWA AANZA ZIARA MIKOA YA KANDA YA ZIWA NA SINGIDA LEO

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akisalimia viongozi wa Jumuia hiyo baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege mjini Bukoba leo kuanza ziara katika mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza na Singida.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo mkoa wa Kagera katika Ofisi ya CCM mkoani humo, leo
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Edmund Mndolwa akizungumza na viongozi hao
Viongozi meza Kuu wakiwa na Dk Mndolwa
Add caption

MWENYEKITI WA CCM RAIS DK. MAGUFULI AONGONZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA (NEC) YA CCM JIJINI DAR ES SALAAM LEO

May 28, 2018

Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli  akiwa meza kuu katika Ukumbi wa mikutano wa Kikwete kwa ajili ya kuongoza Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) leo Jumatatu Mei 28, 2018. Kushoto ni Makamu Mwenyeti wa CCM Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na kulia ni Mamaku Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akitoa hotuba ya utangulizi kwenye kikao hicho
Mwenyekiti wa CCM Rais Dk Mgufuli akiongoza kikao hicho
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho

KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM (NEC) KINACHOENDELEA KUFANYIKA CHINI YA UENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM,DKT JOHN POMBE MAGUFULI KIMEPITISHA MAJINA MAWILI YA WAJUMBE WAPYA WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA NEC AMBAO NI WAZIRI MKUU MSTAAFU WA AWAMU YA NNE NDUGU MIZENGO PETER PINDA NA NDUGU MAKONGORO NYERERE.

KIKAO HICHO PIA KIMEPIGA KURA YA KUWAPATA WAJUMBE SITA  KWA KUZINGATIA JINSIA WATATU KUTOKA TANZANIA BARA NA WATATU KUTOKA TANZANIA ZANZIBAR AMBAO WATKUWA WAJUMBE WA KAMATI KUU

MAJINA 14, TISA KUTOKA KILA UPANDE YALIPENDEKEZWA KUWANIA NAFASI HIZO.
ยช