Rais mteule wa Marekani, Donald Trump
Alkhamisi ya jana alitangaza kuwa, nchi hiyo inapaswa kuimarisha zaidi
uwezo wake wa silaha za nyuklia maadamu ulimwengu haujapata mwelekeo wa
kimantiki kuhusu silaha za atomiki.
Donald Trump hakutoa maelezo zaidi katika uwanja huo lakini
msemaji wake, Jason Miller amesema kuwa, rais huyo mteule wa Marekani
alikuwa akiashiria vitisho vinavyohusiana na uzalishaji na uenezaji wa
silaha za nyuklia na udharura wa kukabiliana na vitisho hivyo hususan
vile vya makundi ya kigaidi katika maeneo yenye machafuko na "serikali
au tawala kigaidi".
Jason Miller |
Trump pia ametilia mkazo suala la kusasisha uwezo wa nyuklia wa
kuzuia vitisho kabla ya kutendeka kama mojawapo ya njia muhimu za
kuimarisha amani.
Matamshi hayo ni ya kwanza rasmi kutolewa na rais mteule wa Marekani
kuhusu silaha za nyuklia za nchi hiyo. Kutangazwa mtazamo huo wa Trump
sambamba na matamshi yaliyotolewa na Rais Vladimir Putin wa Russia
kuhusu uwezo wa silaha za nyuklia wa nchi hiyo ni jambo linalipaswa
kupewa mazingatio maalumu.
Alkhamisi wiki hii pia Rais Putin alitilia mkazo udharura wa kuimarishwa uwezo wa silaha za nyuklia na silaha za kistratejia za Russia na akasema Moscow inapaswa kuimarisha zaidi makombora yenye uwezo wa kufumua na kupasua mfumo wa kujikinga na makombora.
Alkhamisi wiki hii pia Rais Putin alitilia mkazo udharura wa kuimarishwa uwezo wa silaha za nyuklia na silaha za kistratejia za Russia na akasema Moscow inapaswa kuimarisha zaidi makombora yenye uwezo wa kufumua na kupasua mfumo wa kujikinga na makombora.
Taasisi za ulinzi za Marekani na Russia zinasema kuwa, nchi hizo
mbili pekee ndizo nguvu mbili za nyuklia zinazomiliki silaha za
kistratejia za nyuklia katika nyanja tatu za anga, nchi kavu na baharini
na kwa sasa zinasasisha zilaha hizo. Wakati huo huo wataalamu wanasema
kuwa, inatazamiwa kuwa hadi kufikia mwanzoni mwa muongo wa 2040 Marekani
itakuwa imesasisha na kuboresha silaha zake za anga, nchi kavu na
baharini za nyuklia kwa kutumia gharama ya dola trilioni moja. Silaha za
nyuklia za kipindi cha Vita Baridi zingali sehemu muhimu sana ya
stratejia ya ulinzi ya Marekani na maafisa wa nchi hiyo wanasisitiza
udharura wa kulindwa uwezo wa nyuklia wa nchi hiyo.
Katika sera yake ya mshambulizi ya mapema ya silaha za nyuklia,
Marekani imekuwa ikitekeleza mipango kabambe ya kusasisha na kuboresha
zaidi silaha zake za atomiki. Hayo yanafanyika kwa kutumia visingizio
mbalimbali kama vile usasishaji wa silaha za nyuklia katika nchi
wapinzani wa Washington hususan Russia na China ambazo zote mbili
hasahasa Russia, zimetenga bajeti kubwa kwa ajili ya kusasisha silaha
zao za kistratejia za nyuklia. Rusia imeazimia kusasisha na kuboresha
asilimia 70 ya silaha zake za atomiki hadi kufikia mwaka 2020. Hata
hivyo ikilinganishwa na Russia, Marekani ina mipango mikubwa na mipana
zaidi ya kusasisha na kupanua zaidi maghala yake ya silaha za nyuklia.
Marekani ndiyo nchi pekee iliyotumia silaha za nyuklia kuua watu. Hiroshina na Nagasaki, Japan |
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269