Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makala ya
kikosi kazi cha mkoa wa Mbeya kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya mpaka
kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji kati ya Wilaya ya Mbarali
na Chunya (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makala wakati wa
uwasilishwaji wa taarifa ya kikosi kazi cha mkoa wa Mbeya kuhusu
mapendekezo ya marekebisho ya mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na
Vijiji kati ya Wilaya ya Mbarali na Chunya
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza mbele Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makala pamoja na
kikosi kazi chake wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya kikosi kazi cha
mkoa wa Mbeya kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya mpaka kati ya Hifadhi
ya Taifa ya Ruaha na Vijiji kati ya Wilaya ya Mbarali na Chunya
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makala
pamoja na kikosi kazi chake mara baada ya kupokea taarifa ya kikosi
kazi cha mkoa wa Mbeya kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya mpaka kati
ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji kati ya Wilaya ya Mbarali na
Chunya.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
amewaagiza Wakuu wa wilaya nchini kuchukua hatua stahiki katika kulinda
na kuhifadhi mazingira katika wilaya zao ili kukabiliana uharibifu
mkubwa wa mazingira kwenye misitu na vyanzo vya maji ili visikauke na
kuleta athari kwa binadamu na viumbe wengine.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo mara baada ya
kukabidhiwa Taarifa ya Kikosi Kazi cha Mkoa wa Mbeya na Mkuu wa mkoa wa
huo Amos Makalla kuhusu Mapendekezo ya Marekebisho ya mpaka kati ya
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na Vijiji katika wilaya za Mbarari na Chunya -
Ikulu, Jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema tatizo la uharibifu wa
mazingira katika baadhi ya wilaya nchini ni kubwa hivyo kuna umuhimu
mkubwa kwa Wakuu wa wilaya kwa ushirikiano na watendaji wengine katika
kukabiliana na hali hiyo kwenye maeneo yao.
Amesema
kabla ya hatua kuchukuliwa ni vizuri wananchi wakaelimishwa kuhusu
umuhimu wa uhifadhi wa mazingira kabla ya kuondolewa kwenye maeneo
waliyovamia ikiwemo maeneo ya vyanzo vya maji.
Makamu
wa Rais pia amepongeza timu ya wataalamu wa kikosi kazi cha Mkoa wa
Mbeya kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya inayolenga kuokoa mfumo wa
ikolojia katika Bonde la Mto Ruaha Mkuu.
Kwa
upande wake, Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla amemweleza Makamu wa
Rais kuwa aliamua kuunda kikosi kazi hicho kwa ajili ya kushughulikia
mgogoro wa mpaka kati ya wananchi wa wilaya ya Chunya na Mbarali na
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, uharibifu wa mazingira na upotevu wa maji
kwenye Mto Ruaha Mkuu.
Mkuu
wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla baada ya kukabidhi taarifa ya kikosi kazi
kwa Makamu wa Rais amesema kikosi kazi hicho kimependekeza vijiji Tisa
kati ya 33 ambavyo vina mgogoro na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha viondolewe
kabisa kwenye eneo la hifadhi na vijiji vingine Vinne vinatakiwa kufutwa
na wananchi kuhamishwa kwenye maeneo hayo na Serikali itawalipa fidia
na kuratibu eneo watakapohamishiwa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269