Breaking News

Your Ad Spot

Jun 13, 2017

RAIS DK.SHEIN AWAAPISHA MKUU WA JKU NA MKUU WA CHUO CHA MAFUNZO ZANZIBAR


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) akimvalisha cheo cha Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar, Ali Abdalla Ali katika hafla iliyofanyika Juni 13, 2017 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja kabla ya uteuzi huo alikuwa, Naibu Kamishana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha , Ali Abdalla Ali kuwa  Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar  katika hafla iliyofanyika Juni 13, 2017 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja ambapo kabla ya uteuzi huoa alikuwa  Naibu Kamishana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Kanal Ali Mtumweni Hamad  kuwa   Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi, Zanzibar (JKU )  katika hafla iliyofanyika Juni 13, 2017  katika  ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Zubeir Ali Maulid ni miongoni mwa Viongozi waliohudhurika katika hafla hiyo ya kuwapishwa Mkuu wa JKU na Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja .
Baadhi ya Makamanda wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi JKU na Chuo cha Mafunzo Zanzibar wakiwa katika hafla ya kuwapishwa wakuu Wapya na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika Ukumbi wa wa Ikulu Mjini Unguja .
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu (kulia) Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mh .Said Hassan Said na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh, Ayoub Mohamed Mahmoud, ni miongoni mwa Viongozi waliohudhurika katika hafla ya kuwapishwa Mkuu wa JKU na Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mh, Haji Omar Kheri (kushoto) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, ni miongoni mwa Viongozi waliohudhurika katika hafla ya kuwapishwa Mkuu wa JKU na Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbali mbali wa Serikali  baada ya kuwaapisha rasmi  Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Ali Abdalla Ali kuwa (wa nne kushoto) na Kanal Ali Mtumweni Hamad   Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi, Zanzibar  JKU  (wa nne kulia)  hafla iliyofanyika  leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja. (Picha na Ikulu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha Viongozi wa Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), aliowateua hivi karibuni kuwa Wakuu katika Vikosi hivyo. 

Katika hafla hiyo, Dk. Shein kabla ya kumuapisha Naibu Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Ali Abdalla Ali, alimfisha cheo cha Ukamishna na baadae kumuapisha kuwa Kamishna wa Chuo cha Mafunzo, Zanzibar.

Wakati huo huo, Dk. Shein, amemuapisha Kanal Ali Mtumweni Hamad kuwa Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi, Zanzibar (JKU).

Hafla hiyo, ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar  Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za (SMZ), Haji Omar Kheir, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji.

Wengine ni Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud,  Wakuu wa Vikosi vya SMZ, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages