Breaking News

Your Ad Spot

Mar 19, 2010

SALUTARIS LIBENA NA EUSEBIUS NZIGILWA WAWEKWA WAKFU LEO KUWA MAASKOFU WASAIDIZI WA KANISA KATOLIKI JIMBO KUU LA DAR ES SALAAM.


MAASKOFU wasaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Salutaris Libena na Eusebius Nzigilwa wakiwa wamelala kuwekwa wakfu na Askofu Mkuu wa Jimbo hilo, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo (wapili kulia) katika ibada maalumu iliyofanyika leo, Viwanja vya Msimbazi Centre. Kulia ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Askofu wa Jimbo la Dodoma, Jude Ruwa'ichi.ASKOFU Mkuu Jimbo Kuu la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akimkabidhi fimbo maalum ya uchungaji, Askafu Msaidizi wa Jimbo hilo, Salutaris Libena Katika misa ya kuwaweka wakfu Libena na Eusebius Nzigilwa katika ibada hiyo.MAASKOFU wasaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa na Salutaris Libena wakitoa baraka kwa waumini baada ya kuwekwa wakfu.ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycap Kardinali Pengo, akimlisha sakramenti katatifu, Rais mstaafu Benjamin Mkapa wakati wa ibada ya kuwaweka wakfu, Salutaris Libena na Eusebius Nzigilwa kuwa Maaskofu Wasaidizi jimbo hilo.ASKOFU Msaidizi wa Kanisa Jatoliki, Jimbo Kuu la Dar es salaam, Salutaris Libena akimlisha sakramenti takatifu, kaka yake, Kassian Chibogoyo, baada ya askofu huyo kuwekwa wakfu,leo Katika viwanja vya Msimbazi Centre. Libena na Mwenzake Euserbius Nzugulwa walitakiwa kulisha sakramenti hiyo ndugu zao kwanza ndipo waendelee kwa weumini wengine.RAIS mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Mama Anna wakishiriki kaika ibada hiyo. katikati yao ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Philip Marmo aliyemwakilisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa niaba ya serikali kwenye ibada hiyo.BAADHI ya waumini wakiwa katika ibada hiyo.WATOTO waliovalia rasmi wakiwa kwenye ibada hiyo.moja ya vipeperushi vilipokuwa vikigawiwa waalikwa kwenye ibada hiyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages