.

DUDUMA ATANGAZA NIA YA KUMG'OA MANENO JIMBO LA CHALINZE

Apr 22, 2010

*ASEMA ANAZO NONDO ZA KUTOSHA KUUTWAA UBUNGE AKITEULIWA NA CHAMA
NASSOR HUSSEIN DUDUMA
MPIMAJI na ramani Mkuu wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Nassor Duduma ametangaza nia yake ya kutaka kugombea ubunge jimbo la Chalinze mkoani Pwani.
    Duduma alitangaza nia hiyo jana kwenye Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Bagamoyo kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na kutaka kuwapa maendeleo zaidi wananchi wa jimbo hilo ambalo kwa sasa nipo chini ya Ramadhani Maneno.
    Mgombea huyo aliongeza kwamba amefikia maamuzi hayo kuwa amegundua ana sifa za kutosha kuwania hiyo ikiwemo elimu,uzoefu wa kiutendaji kiasia katika Chama na Serikali ndani ya nje ya nchi.
   Aliongeza kuwa sababu nyingine ni pamoja na kutaka kutumia haki ya demokrasia ambayo inawapa wanacnhi kuchagua kiongozi wanayemtaka kwa ajili ya kuwaletea maendeleo katika jimbo hilo.
   Duduma alisema kuwa pia amefikia uamuzi huo baada ya kufanya majadiliano na baadhi ya wakazi wa jimbo hilo na kuonesha nia ya kumuunga mkono kuwania nafasi hiyo ili aweze kusimamia sera,na mambo mengi katika jimbo na nchi kwa ujumla.
   Mgombea huyo alisema kuwa jambo jingine lililo mfanya aweke nia hiyo ni kutaka kusimamia mpango kazi ambao ameuandaa kwa ajili ya kuyaenzi mambo mazuri yaliyofanywa na viongozi waliotangulia na kuyafanyia kazi yake yote yaliyoshindikana kwa sababu mbalimbali.
  Sambamba na nia hiyo,Duduma alieleza kwamba atashirikiana vyema na viongozi na Serikali kuhakikisha anasimamia kazi mbalimbali zikiwemo kutunga sheria,kuishauri serikali na kusimamia majukumu mbalimbali.
   Pia alisema kwamba jambo jingine ambalo limemvuta zaidi kuwania nafasi hiyo ni kutaka kupiga vita na kukemea aina yoyote ya ubaguzi wa rangi,unyanyasaji wa jinsia ,kupigania haki ya mwanamke kujikomboa na vita vya matumizi ya madawa ya kulevya na ugonjwa wa Ukimwi.
   Duduma ambaye ni Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa tokea mwaka 2007 hadi 2012 amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika Taasisi mbalimbali zikiwemo Chama cha wafanyakazi(TUGHE)Katibu wa Tawi la chama hicho Ardhi 1997 hadi 1998 na mjumbe wa mkoani wa Morogoro,1987 hadi 1998.
     Mkurugenzi wa ufundi na kaimu katibu Mkuu wa klabu ya Yanga,2003 hadi 2005,Mkurugenzi wa mradi wa viwanja wa manispaa ya Temeke mwaka 2007 hadi 2008 na mjumbe wa Baraza la taifa la wapima ardhi Tanzania (NCPS)kuanzia 2007 hadi sasa.
    Pia mgombea huyo anashikiria nafasi ya Katibu wa Chama cha Wapima ardhi (IST)tokea mwaka 2004 hadi sasa,mjumbe wa mkutano mkuu CCM (w) ya Bagamoyo tokea 2007 hadi 2012
Duduma akitangaza nia yake leo, katika Ofisi ya CCM wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani. Kushoto ni Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Fikirini Masokolo na wapili ni Mwenyekiti wa Chama wilaya hiyo, Omar Kabamba

JINA: NASSOR HUSSEIN DUDUMA
ANUANI:  SLP 61953, DAR ES SALAAM
SIMU: 0713/0786/0766-214533
E-MAIL: duduma@yahoo.com
KUZALIWA: BUNBULI-LUSHOTO TANGA
RAIA: MTANZANIA KWA KUZALIWA

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช