.

MWALIMU SHULE YA MSINGI ATAKA UBUNGE WA SIKONGE

Apr 23, 2010

JOYCE akizungumza na mkono wetu,  ambapo alionyesha kuwa na duduku la kueleza kwa kina kwa nini ameamua kusaka ubunge. Chini ni picha zaidi zinazoonyesha hisia aliyokuwa nayo.Akaishia hapa, sasa stori yenyewe ndio hii dauni
MWALIMU wa Shule ya Msingi Kipunguni, Joyce Ibrahimu ametangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Sikonge, mkoani Tabora.
   Joyce alitangaza nia hiyo jana ya kumvaa Ubunge wa jimbo hilo, Said Nkumba (CCM), katika ofisi za gazeti hili zilizopo mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam.
   Alisema ana nia ya dhati ya kugombea jimbo hilo kutokana na uchungu alionao kwa wananchi hao ambao bado wapo nyuma kimaendelea licha ya kuwa na ardhi nzuri yenye rutuba.
  Joyce alisema wananchi hao wameachwa nyuma bila sababu yeyote na kwamba akiwaangalia wanawake walivyo na wasichana wanaacha shule kutokana na wazazi wao kutokuwa na uwezo anapatwa na uchungu zaidi.
   Alisema kutokana na uzoefu alioupata kutoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), akiwa Mwenyekiti wa CWT, kitengo cha wanawake mkoa wa Dar es Salaam na katika Wilaya ya Ilala, anaamini anaweza kuwasaidia wananchi wa jimbo hilo.
  Joyce alisema hajisikii vizuri kuona jimbo hilo na watu wake wanaendelea kuwa maskini kama hawana kipato na kuishi maisha duni wakati wana vyanzo vya kutapata utajiri.
  Alisema jimbo hilo lina vyanzo vingi vya uchumi na mapato kutokana na kulima karanga, ufuta na tumbaku ambavyo vinaweza kuwaingizia mapato.
   Pia, alimpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuweka historia ya kuwa rais wa kwanza kukanyanga ardhi ya tarafa ya kitunda, mkoani Tabora.
   Alisema mara ya kwanza Rais Kikwete alikwama kwenda katika tarafa hiyo lakini mara ya pili alidhamilia kwa dhati hadi alifika katika eneo hilo.
  Joyce alisema kutokana na kitendo alichoonyesha kwa wapiga kura wake anastahili kupongezwa na ameona adha ya jimbo hilo ilivyo kutokana na miundombinu mibaya ya barabara.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª