Breaking News

Your Ad Spot

May 22, 2010

KILI TAIFA CUP, TBL HAIHUSIKI NA MASUALA YA KIUFUNDI

NI TAMKO LA EXECUTIVE SOLUTIONS LTD

TAARIFA KAMILI
Ndugu wanahabari wenzangu,
    Napenda kutumia nafasi hii kwanza kuwapa pole kwa kazi. Najua mnayo majukumu mengi kuhakikisha Watanzania hasa wapenda michezo wanapata habari kwa wakati unaostahili.
    Pia natoa shukrani za dhati kwa ushirikiano mkubwa tunaopata kutoka kwenu katika shughuli zetu za kila siku hususani kwenye mashindano yanayoendelea ya Kili Taifa Cup.
   Japokuwa mashindano ya mwaka huu yamefana kuna mambo kadhaa yamejitokeza kama vile baadhi ya timu za mikoa ya Mara na Ruvuma kukata rufaa baada ya kutoridhika na uamuzi uliotolewa na Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) kutokana na timu ya Mara kudaiwa kuchezesha mchezaji ambaye hakukidhi masharti ya mashindano na Ruvuma kudai kuwa Lindi ilichezesha wachezaji wa aina hiyo pia. Rufaa hizi zinasikilizwa na TFF.
   Baadhi ya magazeti yanaandika kuhusu suala hilo na pia vituo vya redio na TV vinarusha habari zinazohusiana na suala hilo na baadhi kumhusisha mdhamini wa mashindano hayo na masuala ya kiufundi ya mashindano hayo.
   Executive Solutions, tukiwa wakala wa TBL kuratibu masuala ya habari katika mashindano haya, tunapenda kufafanua kwamba Kilimanjaro Premium Lager haihusiki kabisa na masuala ya kiufundi ya mashindano haya. Mashindano yanaratibiwa na TFF kwa asilimia mia moja.
  Kama kuna jambo lolote munahitaji kufahamu zaidi, nawaomba wanahabari wenzangu musisite kuwasiliana na TFF au Executive Solutions kwa ufafanuzi zaidi.
   Nitawatumia taarifa kamili kuhusu mashindano haya mara baada ya TFF kutoa uamuzi kuhusu rufaa mbili zilizotolewa. Bado wanaendelea na kikao.

Natanguliza shukrani,

Michael Mukunza
Media Manager
Executive Solutions Ltd
P.O. Box 1601, Dar es Salaam
Mobile: 0784/0776/0767978302 or 0714683451

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages