Breaking News

Your Ad Spot

May 5, 2010

MHASIBU ASHINDA MISS UTALII TANZANIA –VYUO VIKUU 2010 –KANDA YA KASKAZINI NI ADELQUEEN JOSEPH NJOZI

Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo cha uhasibu cha Arusha,Adelqueen .J.Njozi,mwishoni mwa wiki afanikiwa kutwaa taji la Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu 2010 –Kanda ya Kaskazini na kujinyakulia shilingi milioni moja na laki tano kutoka Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na kidani cha Tanzanite cha shilingi milioni moja toka Culture Heritage. Katika shindano hilo lililokuwa na ushindani mkali,mshindi aliwashinda washiriki wengine kumi kati ya kumi na moja walioshiriki shindano hilo.Mshindi wa pili alikuwa ni Judith Elitwaza aliye zawadi za shilingi milioni moja toka Mamlaka ya Hifadhi za taifa (TANAPA),wa tatu alikuwa Zena Nasib aliye zawadi za shilingi laki nane toka Intergance Securico,wanne ni  Anitha Mbowe aliye zawadi za shilingi laki tano toka Modern Ricks Club,watano ni Zainab Rajabu aliye zawadi za shilling laki tatu toka Mwandago Investment na mshindi wa tuzo ya Vipaji ni Grace Temba aliye zawadiwa shilingi laki nne toka Supreme Power Fance.Warembo ambao hawakushinda nafasi yoyote ni Omega Maoki,Beatrice Discoryce,Beatrice Ngowi,Sallome Kessy,Restuta Vedasto ambao kila mmoja alizawadiwa shilingi elfu hamsini zilizo tolewa kwa pamoja na Empire Sports,Victoria Expediation,Aquline hotel,Business Times Limited,Naipenda Safari,QX Club.
   Maelfu ya watu waliohudhuria shindano ,wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mheshimiwa Isdori Shirima katika ukumbi wa hoteli ya kitalii ya Naura Springs Hotel,walijikuta wakishangilia kila warembo hao walipopita jukwaani wakiwa katika mavazi ya Ubunifu,Kutokea,Kitalii na ya Asili ,huku ukumbi mzima ukizizima kwa nderemo na vifijo wakati warembo hao walipoingia jukwaani kila mmoja akiimba na kucheza ngoma na nyimo halisi za makabila ya Tanzania wakiwania tuzo ya Vipaji.
   Msanii wa kizazi kipya Barnaba aliongoza burudani zilizosindikiza shindano hilozikiwemo Mwanamziki Ndanda Cosovo,Belle 9 na kundi la ngoma za asili ambalo lilitia fora kwa ngoma za asili za mikoa ya Arusha na Lizombe ya mkoa wa Ruvuma.
   Akihutubia katika shindano hilo,mkuu wa Mkoa wa Arusha Isdori Shirima,aliwapongeza sana waanzishi na wabunifu wa shindano la Miss Utalii Tanzania,kwa kubuni shindano linalozingatia mila na utamaduni wa Kitanzania na lenye kutangaza utalii na utamaduni wa mtanzania,huku akiyataka mashindano mengine kuiga mfano wa shindano la Miss Utalii Tanzania. “Leo ni mara yangu ya kwanza kuhudhuria mashindano ya urembo,na nimehudhuria baada ya kuhakikishiwa kuwa shindano hili ni tofauti nay ale mengine yanayo tumia utamaduni wa kigeni ambao kwa kiasi kikubwa ni adui wa utamaduni wetu” alisema mkuu huyo wa mkoa,aliongeza kuwa kukubali kwake kuwa mgeni rasmi kumetokana na kuthamini mchango wa shindano hilo katika sekta ya utalii na utamaduni,pia kutokana na umuhimu wa sekta ya utalii na utamaduni kwa Taifa katika kupambana na umasikini na tatizo la ajira. Alitoa wito kwa wasomi ,hususani mabinti kutumia fulsa mbalimbali zinazo patikana kama hii ya Miss Utalii Tanzania kutangaza utalii na utamaduni wetu kitaifa na kimataifa.
   Akizungumza baada ya shindano hilo,Mkuu huyo wa mkoa alielezea kuridhishwa kwake na shindano la Miss Utalii Tanzania,na kutoa wito kwa waandaaji wa taifa kuipa Arusha heshimwa ya wenyeji wa fainali za Taifa mwaka huu “shindano hili ni kielelezo cha urithi wa Taifa,hazina ya utamaduni wetu na tafsiri ya vitendo ya sera za Taifa za Utalii na utamaduni pia uungaji mkono wa juhudi za serikali katika sekta ya utalii na utamaduni” aliyataka makampuni na mashirika mbalimbali kusaidia kudhamini shindano hili ,akiamini kuwa iwapo wadhamini wakubwa watajitokeza basin chi yetu itakuwa na namna ya shindano la kujivunia kitaifa na kimataifa.
   Wadhamini wakuu washindano hilo,ambalo pia lilihudhuriwa na rais wa mashindano hayo nchini Gideon Chipungahelo ni pamoja na Naura Springs Hotel,Mamlaka ya Hifadhi za Taifa(TANAPA),Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA),Modern Ricks Club,Business Times Limited,Mwandago Investments,Aquline Hotel, Intelligence Securico, Supreme Power Fence,QX Pub,Culture HeritageSnow crest hotel,Vero Salon na Empire Sports.
Regard

Erasto Gideon Chipungahelo
President of Miss Tourism Tanzania & Miss Heritage World Organisation
+255 773 318 278 ,715 318 278,754 318 278

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages