Breaking News

Your Ad Spot

May 21, 2010

OSAKA STORES LTD YAKABIDHI NYUMBA ZA CHUO CHA MAOFISA WAKUU WA POLISI KIDATU

Ni ilizokarabati kwa zaidi ya sh. milioni 331 MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni  ya Osaka Stores Ltd ya mjini Dar es Salaam, Edson Mwakatobe (kushoto), akimkabidhi funguo Kamishima Msaidizi wa Polisi Kikosii cha Ujenzi, Rochard Malika katika hafla ya kampuni hiyo kukabidhi kwa jeshi hilo nyumba kumi, vyumba  viwili vya madarasa ilivyofonyia ukarabati mkubwa, katika Chuo cha Maofisa Wakuu wa Polisi, Kidatu mkoani Morogoro. Sherehe hiyo ilifanyika  chuoni hapo, jana.. Wapili Kulia ni Mkuu wa chuo hicho, Kamishna Msaidizi Ally Lugendo na Wa tatu ni Msimamizi Mkuu wa Ujenzi makao makuu ya jeshi hilo, Mrakibu Mwandamizi, John Muyela.
Mwakatobe akisoma taarifa ya kukamilika kwa mradi wa ukarabati wa nyumba hizo, vyumba viwili vya madarasa ambao umegharimu jumla ya sh. milioni 331.4. Kulia ni Msimamizi Mkuu wa Ujenzi makao makuu ya jeshi hilo, Mrakibu Mwandamizi, John Muyela. VIONGOZI kutoka makao makuu ya polisi wakikagua chumba cha darasa kabla ya makabidhiano hayo.
KAMISHNA Msaidizi wa Polisi Kikosi cha Ujenzi cha jeshi hilo, Malika, akikagua sehemu ya taa katika BAADHI ya nyumba zilizofanyiwa ukarabati na kampuni hiyoMFANYAKAZI akisafisha mazingira ya moja ya nyumba hizoMkurugenzi wa Osaka na wafanyakazi wa kampuni hiyio wakikagua kabla ya kukabidhi

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages