Breaking News

Your Ad Spot

Jul 10, 2010

DK SHENI APITA KUWA MGOMBEA URAIS Z'BAR KWA TIKETI YA CCM

Hatimaye Makamu wa Rais, Dk Ali Mohammed Sheni amepita kuwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu baada ya kuchaguliwa kwa kura 117  na kuaacha mbali waziri Kiongozi mstaafu Dk. Mohamed Gharib Bilal aliyepata kura 54 na waziri Kiongozi wa sasa,  Shamsi Vuai Nahodha aliyepata kura 33, katika uchaguzi wa kinyang'anyiro hicho uliofanywa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa taifa (NEC) ya CCM  jana usiku katika ukumbi wa Kizota mjini Dodoma.

Dk. Sheni amepenya baada ya kuingia wakiwa watatu waliopenya awali katika mchujo wa Kamati Kuu wa CCM lakini akiwa pia katika wale watano waliokuwaa wamependekezwa na Kamati maalum Zanzibar, kati ya jumla ya makada 11 waliochukua fomu na kuzirejesha kuwania nafasi hiyo inayoachwa ana rais wa sasa Amani Abeid Karume.Dk Ali Mohammed Sheni akizungumza baada ya kuchaguliwa
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Dk. Shein baada ya ushindi wake. Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Dk. Gharib Bilal kwa kukubali matokeoBaadhi ya wajumbe wakiwa katika kikao cha NEC. Kushoto ni Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha aliyekuwa akiwania nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages