Breaking News

Your Ad Spot

Sep 6, 2010

MICHUANO YANETIBOLI KUFUZU KUCHEZA KOMBE LA DUNIA YAANZA LEO MJINI PRETORIA SAUZI

Michuano ya kusaka nafasi kucheza kombe la dunia mwaka 2010 imeanza leo katika jiji la Pretoria NCHINI AFRIKA KUSINI ambapo TANZANIA imeanza vyema mashindano hayo kwa kushinda mechi yake kwa kwanza kwa magoli 50 kwa 25 dhidi ya Lesotho.

TANZANIA ilionyesha kiwango kizuri katika mashindano hayo kutokanana kucheza mchezo wenye ujuzi mkubwa ambapo iliweza kuisambaratisha LESOTHO .
          Akifungua mashindano hayo naibu waziri wa michezo wa AFRIKA KUSINI GERT OOSHIZEN amesema kuwa mashindano hayo yanaimarisha mchezo huo na kuweka ushuaino mzuri baina ya nchi zinazoshiriki.
          Mchezo mwingine ulikuwa kati ya ZIMBABWE na AFRIKA kusini ambapo timu hizo zimeonyeshana kazi kubwa kutokana na kila timu kujiandaa vilivyo ambapo AFRIKA KUSINI iliibuka mshindi kwa magoli 64 kwa 29.
         Kwa upande wake kocha wa TANZANIA SIMONE MCKIWIS amesema a mefuahia ushindi wa timu yake na kuanhidi watanzania kuwa timu hiyo itaendeela kufanya katika michezo yake inayoendeela ambapo amewataka watanzania kuiunga mkono timu hiyo.
         Hata hivyo mashindano hayo yamekosa msisimko mkubwa kutokana na mashabiki wachache kuhudhuria, tofauti na mashindano ya kimataifa yaliyofanyika nchini mwaka jana ambapo watu mbali mbali waliweza kuhudhuria.
        Mashindano hayo yanashirikisha timu sita kutoka AFRIKA ambazo ni NAMIBIA,TANZANIA,BOTSWANA,LESOTHO,ZIMBABWE, na wenyeji AFRIKA KUSINI.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages