Breaking News

Your Ad Spot

Oct 1, 2010

JK ATUMA SALAM, MIAKA 50 YA UHURU WA NIGERIA

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amempelekea salaam za pongezi Rais wa Nigeria Dakta Goodluck Ebele Azikiwe Jonathan kwa kutimiza miaka 50 ya uhuru wa nchi yake.
      Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imesema katika Salaam zake, Rais Kikwete amempongeza Rais huyo kwa niaba ya wananchi wa Tanzania kwa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa taifa la Nigeria.
Rais Kikwete alisema Serikali yake inathamini sana uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya wananchi wa nchi hizi mbili ulionzishwa na wanzilishi wa mataifa haya yote mawili.
“Tafadhali pokea salaam na pongezi zangu za dhati Mhe. Rais na ninapenda kukutakia maisha marefu yenye afya njema” alisema Mhe. Rais katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa.
Leo tarehe 1 Oktoba, 2010, taifa la Nigeria linatimiza miaka 50 ya uhuru wake. Katika sherehe iliyoandaliwa na Ubalozi wa Nigeria hapa nchini, Waziri wa Wizara inayoshughulikia uhusiano wa Jumuiaya ya Afrika Mashariki, Mhe. Diodorus Kamala atakuwa mgeni rasmi

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages