UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Ndugu Martin Shigela, kufuatia kifo cha ghafla cha Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM wa Wilaya ya Musoma Mjini, Ndugu Wilfred Peter Muga.
Ndugu Muga (32) alipoteza maisha yake wakati basi alimokuwa akisafiria kwenda Kigoma kushambuliwa na majambazi jana, Jumapili, Novemba 21, 2010. Ndugu Muga amezikwa mjini Kigoma leo, Jumatatu, Novemba 22, 2010.
Katika salamu zake, Mwenyekiti Kikwete amemwelezea Muga “kama kijana ambaye alikuwa ameufanyia mengi Umoja wa Vijana katika kipindi alipoajiriwa na Umoja huo.”
Muga aliajiriwa kama Katibu wa Vijana wa CCM wa Wilaya Oktoba mosi, mwaka 2006, na katika miaka yake minne ya utumishi wa Vijana amekuwa Katibu wa Wilaya wa Chato na Bukoba Mjini, Mkoani Kagera kabla ya kuhamishiwa Musoma Mjini mwanzoni mwa mwaka jana.
Ameongeza Mheshimiwa Kikwete: “Umoja wa Vijana umepoteza kijana hodari, mwenye kujituma na mwenye mapenzi makubwa na Umoja wa Vijana na Chama cha Mapinduzi. Tumempoteza katika mazingira ya kusikitisha sana wakati tulipokuwa bado tunamhitaji na kuhitaji utumishi wake.”
“Kupitia kwako, Katibu Mkuu wa UVCCM, napenda pia kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya Ndugu Muga. Nawaomba subira katika kipindi hiki kigumu. Nataka wajue kuwa tuko nao katika kipindi hiki cha huzuni na maumivu makubwa lakini yote ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
22 Novemba, 2010
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269