Breaking News

Your Ad Spot

Nov 22, 2010

MBIO ZA UMEYA: WALIOCHUKUA FOMU ILALA WAKAMILISHA KUZIJAZA NA KUZIAREJESHA

JUMLA la madiwani wateule wanne waliochukua fomu za kugombea umeya katika manispaa ya Ilala wamerudisha fomu hizo.

Kwa mujibu wa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ilala Ernest Chale alisema wagombea wote waliochukua fomu kwake wamerudisha isipokuwa Hashim Sagafu. Chale alisema hayo leo alipokuwa akizungumza na Chachandu Daily, mjini Dar es Salaam .

Alisema kuwa waliomba nafasi ya unaibu meya ni wawili ambao ni diwani wa Kisutu, Kherry Kessy na Abdulkarim Masamaki wa Kariakoo na tayari wamesharudisha fomu zao.

Chale aliwataja wengine waliochukua fomu na kurudisha ambapo kata zao zipo katika mabano kuwa ni Jerry Silaa (Gongo la Mboto), Salum Bisakala (Gerezani) na Dk. Didas Masaburi (Kivukoni)


Alisema uchukuaji wa fomu hizo ulianza Novemba 20 na ulimalizika jana saa 10 jioni ambapo alisema baada ya kumalizika kwa mchakato huo majina hayo yatapelekwa katika kikao cha utendaji cha kamati ya siasa ya wilaya kwa ajili ya kujadiliwa.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages