Breaking News

Your Ad Spot

Feb 3, 2011

MKUTANO WA WADAU WA NSSF MJINI ARUSHA LEO

VIONGOZI wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakijadiliana jambo, kabla ya kuanza mkutano wa kwanza wa wadau wa shirika hilo, leo katika ukumbi wa Simba, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (IACC) mjini Arusha.  Kutoka kushoto ni Mkurugnezi wa Uendeshaji Crescentius Magori, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamnini wa Shirika hilo, Abuabakari Rajabu. 
Kaimu Katibu Mkuu wa TUCTA,  Nicholaus Mgaya (kushoto) akijadili jambo na Nicholaus Kingazi kutoka Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) wakati wa mkutano huo leo 
Mkuu wa  Uhusiano na Huduma kwa wateja, Eunice Chiume (kulia) akijadiliana jambo na maofisa wengine wa NSSF kabla ya mkutano wa leo kuanza. 
MJUMBE wa Bodi ya wadhamini ya NSSF, Mudhihir Mudhihir (kushoto), akizungumza na Mbunge wa Ilala, Mussa Hasaan Zungu na Mkuu wa Uendeshaji wa NSSF, Crescent  Magori  wakati wa mkutano huo. Zungu alitarajiwa kutoa mada kuhusiana na mradi wa ujenzi wa makazi ya kisasa utakaofanywa na NSSF eneo la Mchikichini, Dar es Salaam. 
OFISA wa NSSF, Makene Magoti akiwa na Ofisa Itifaki na Uhusiano wa Kituo cha AICC kabla ya mkutano kuendelea leo. 
Mikonoz wa NSSF wakiwa ukumbini

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages