"Hii itapunguza mgawo wa umeme kwa sasa kwa megawati zipatazo 70", alisema Injinia huyo ambaye alifuatana na Meneja Uhusiano wa Shiruika hilo, Badra Masoudi (kulia) na kuongeza "tunatarajia kwamba msimu wa mvua za masika utaanza punde, na hii itafanya uzalishaji wa umeme katika mitambo ya maji kuongezeka na hivyo kuliondoa tatizo hilo kwa sasa.
"Pia Shiruka linawasiliana na serikali kuangalia uwezekano wa kupata mit ambo ya dharura ili kukabiliana na hali inayoweza kujitokeza endapo mvua za masika zitakuwa chini ya wastani unaotarajiwa", akasema Injinia Mramba.
Akasema, uongozi wa Tanesco unawaomba radhi sanaaaa, wananchi kutokana na usumbufu mkubwa unaotokana na adha ya mgawo huo wa umeme na pia Shirika linawasihi wananchi kushirikiana na shirika hilo, na kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu cha upungufu wa umeme.
"Tunaahidi kwamba tutafanya kila jitihada kurekebisha mapungufu balimbali ambayo yamekuwa yakijitokeza hapa na pale katika utekelezaji wa zoezi hili la mgawo hasa kudhibiti matukio ya dharura yanayofaya ratiba zisifuatwe kama zilivyopangwa", akamaliza..
******************************************
KABLA YA MKUTANO KUANZA, BAADA YA WAANDISHI WA HABARI KUKAA KATIKA OFISI ZA TANESCO KWA ZAIDI YA SAA MBILI WAKISUBIRI KUANZA KWA MKUTANO HUO MAMBO YAKAWA HIVI...........
Waandishi hawa wakakaa 'high table' na kusema, "ndugu waandishi wa habari, tumewaita leo kuzungumzia hali ya mgawo wa.... lakini bahati mbaya tumechelewa kuanza... Haya ulizeni maswali...(Kicheko)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269