Breaking News

Your Ad Spot

Feb 2, 2011

WAZIRI KABAKA AMWAKILISHA PINDA UFUNGUZI MKUTANO WA WADAU WA NSSF

WAZIRI wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, akisindikizwa na wenyeji wake kwenda ukumbini, baada ya kuwasili kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha AICCM mjini Arusha, ambako alifungua mkutano wa wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)  kwa niaba ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF, Abubakari Rajabu na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Raymond Mushi. 
WAJUMBE wakiwa kwenye mkutano wa wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ulioanza leo katika ukumbi wa Simba, kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha AICC mjini Arusha. 
WAZIRI wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akimkabidhi tuzo, Mstaafu anayeishi wa pensheni ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Joram Areray, leo, baada ya kufungua mkutano wa kwanza wa NSSF, katika ukumbi wa Simba, kwenye kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha AICC mjini Arusha. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau na wapili ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF, Abubakari Rajabu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages