Breaking News

Your Ad Spot

Mar 9, 2011

SIKU YA FIGO DUNIANI,WATU KIBAO WAJITOKEZA KUPATA HUDUMA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA LEO

Mkazi wa jijini Dar es Salaam, Ali Bwamkuu ambaye pia anafahamika kama shabiki mkubwa wa timu ya Yanga, akipimwa urefu na Dk. Amir Juya wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ikiwa ni moja ya hatua za kupimwa figo, huduma ya upimwaji figo, moyo na kisukari ilipotolewa aleo kwenye Viwanja vya Mnazi moja, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Figo duniani.
Salma Hemed akiwa na mtoto wake Latifa Jumanne (aliyelala), ambaye alimleta kupata  kupimwa figo, kwenye viwanja hivyo. kwa mujibu wa mama, Latifa ana uvimbe tumboni.
Mtaalam wa Lishe kutoka Kenya, Alice Ochieng (kulia) akitoa somo kuhusu jinsi vyakula vinavyoweza kuwa chanzo cha magonjwa ikiwemo ya figo, kabla ya kuwapatia huduma waliojitokeza kupimwa figo, kwenye viwanja hivyo vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Mmoja wa wananchi waliofika kupata huduma na kuhudhuria semina hiyo kwanza, akiuliza swali kupata ufafanuzi kuhusu nini chanzo hasa cha ugonjwa wa figo.

Watu wakiwa katika foleni ili kupata huduma ya kupimgwa figo kwenye viwanja hivyo vya Mnazo Mmoja. Upimwaji huo na huduma zote ni bure. (Picha Zote na Chachandudaily.blogspot.com).

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages